
Usichanganye kati ya sheria za Mungu na uoga wako wa maisha
Usihusishe kabisa mila na tamaduni kisa uoga wako mwenyewe
Wanawake wengi sana wanateseka mno kwenye ndoa zao kwa kisingizio cha Mungu
Wengine huogopa macho ya watu, ndugu mila na tamaduni zao
Sio kwamba wanapenda kukaa kwenye ndoa walizopo!
Mama yangu alikuwa muhanga wa ndoa za maumivu na mateso
Alikaribia kunisababishia kifo kisa ndoa yake
Mara baada ya kuachana na baba yangu mzazi, jamii ilimuandama sana
Eti kwanini aliomba talaka yake! Licha ya kupitia mateso kwa baba yangu
Yani walitaka avumilie mateso kisa mwanamke hupaswa kuwa mvumilivu!
Kwahio baada ya kuachika alitafutiwa mume mwingine na akaolewa kwa nguvu
Yule mume alikuwa na wake wengine 2 pamoja na mama jumla wanawake 3
Maisha ya yule mwanaume yalikuwa magumu sana kama mnavyojua mashekhe au tuseme walimu wa madrasa
Alikuwa na wake 2, watoto zaidi ya 15 na hali duni sana ya maisha
Na bado hakutaka mke wake yoyote afanye kazi au biashara yoyote ile
Kula ilikuwa mara1 tu kwa siku tena chakula tuligombania kama sandakalawe! na mwenye nguvu pekee ndio angalau hupata ujazo kidogo wa shibe
Mama alikuwa muhanga wa mateso ya ndoa kuanzia kwa mume mpaka wake wenzake kama mnavyojua ndoa za mitala
Ila aliogopa kuachika kwasababu ya macho ya watu na vitisho vya wazazi na ndugu zake!
Kuna siku niliumwa sana homa kali mno, baada ya kupelekwa hospitali na kuandikiwa dawa mama hakuweza kununua
Gharama ilikuwa elfu 1000 tu za kitanzania Ila hakuwa hata na mia nyekundu wala mume hakutoa msaada
Kama mnavyojua hospitali za serikali dawa utaambiwa zimeisha licha ya kuwepo!
Hivyo mama alirudi akiwa na mawazo mengi mno huku hali yangu ikiwa mbaya sana
Ndio akapata mawazo ya kuomba msaada kwa babu yangu aninunulie dawa
Ila babu (upande wa ubabani kwangu) aliamua kuni chukua na kunilea kisha yeye kubaki kwenye ndoa yake
Yani mama alikaribia kunipoteza kisa ndoa! Au tuseme uoga wa kuachika endapo angefanya biashara yoyote kujikwamua
Mama alikaribia kuniua kwa homa kisa ndoa yake na macho ya watu waliomsimanga kwanini aliachika ndoa ya kwanza!
Mama angesababisha kifo changu kisa ndoa ambayo haina msaada wowote ule
Au tuseme sheria ya Dini inataka mwanamke amtii mume wake je, ningekufa Mungu angelipokea katika namna gani hilo?
Je, mama yangu angebaki anasema nimekufa kwa Mapenzi ya Mungu au angejilaumu kwa kufuata sheria za dini yake?
Wakati mwingine madhara mengi hutokea kwa watu kufuata sheria ambazo hazina uhalisia
Uoga wa kusemwa au kwenda nje ya mila na tamaduni zimepelekea vifo vya watu wengi sana
Wanawake wanaishi kwa kufuata Kauli za wanaume zao, Kauli ambazo huua ndoto na malengo yao kisa ndoa!
Ndoa zimejaa maumivu na machungu mengi mno kila kukicha
Ila wanaogopa kutoka au kusema kisa watapoteza wanaume kana kwamba hao wanaume ndio pumzi zao.
Shtuka! Kama ndoa haina heshima wala kukupa nafasi ya kupigania malengo yako, hio haifai kuwa ndoa.