Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Kama Umefanikiwa Angalau Kidogo Na Una Mama Yupo Hai Basi Mtunze Sana Mama Yako

Mama yangu kipenzi (Mungu amrehemu huko alipo) aliwahi kunipambania sana,

Kwa wakati ule sikujua kwa namna gani mama anateseka kwa ajili yangu,

Akili za utoto huwa tunaona kila jambo rahisi sana na pia huwa tunawapa wazazi mtihani pale tunapotamani vitu nje ya uwezo wao

Mama alikuwa masikini tu kama wa mama wengine (aliolewa ndoa nyingine baada ya kuachana na baba)

Yule mume mpya hakutaka wake zake wafanye kazi (alikuwa na jumla ya wake 3 na hana maisha yoyote zaidi ya kufundisha madrasa ndogo)

Hivyo hali ilikuwa ngumu sana pale nyumbani tulipokuwa tunakaa,

Mama hakuwa na pesa, alikuwa mweupe peee na hata hawezi kununua chochote kwa uwezo wake mwenyewe

Nakumbuka kuna kipindi mke mkubwa aliwanunulia wanae mabegi mapya ya shule (sio mabegi serious, ni ile mifuko kwa wale wa zamani wanajua, ilikuwa imeandikwa spots kwa nyuma)

Enzi zile watoto wengi waliipenda sana yani kila mtoto anataka kuwa na ile mifuko hata mimi nilikuwa mmoja wao.

Baada ya wenzangu kununuliwa na mama yao, mimi pia nililia sana kwa mama nataka begi (bei ilikuwa shilingi Mia 300 tu kama sijakosea)

Ila mama hakuwa na uwezo (sio utani hii imetokea kwenye maisha ya mama yangu kabisa)

Sikujua kama mama hana pesa Ila nilihisi hataki tu kunipa, kumbe mama alikuwa anaumia sana ndani kwa ndani kuona nalia kila siku,

Wote tunajua upendo wa kina mama kwa watoto zao, so hata mama yangu alinipenda sana( baba yangu mzazi alikuwa mbali yaani dar es Salaam na sisi tulikuwa kigoma pia hakuwa na mawasiliano na mama tena hata simu mama hakuwa nayo kwa wakati ule).

Siku moja mama aliniambia tutaenda sehemu kuchukua mabegi, eti kuna mtu anagawa mabegi kama yale hivyo nisijali

Kweli bwana, siku ikafika mama akanichukua kwenda huko kupewa begi

Kumbe mama alikuwa anaenda kuomba msaada kwa ndugu yetu mwingine (😭😭😭) this is so painful to me kila ninapokumbuka

Sikujua kabisa kwa namna gani mama anataka kunifurahisha na kwa namna gani mama ana hali mbaya kiuchumi (kisa ndoa isiyo na tija)

So tulienda aise umbali ni mrefu sanaa yani tulitembea umbali mkubwa sana kiasi njiani nilishindwa na mama kulazimika kunibeba (hata nauli hakuwa nayo masikini mama yangu, kumbuka enzi hizo nauli ilikua kama shilingi mia moja yaani tsh 100) kama sijakosea

Tulifika kweli na mama alipata begi lile (sema tayari lilikuwa limetumika)

Yule ndugu wa mama alikuwa na uwezo kidogo hivyo mama aliomba kisanii begi hakusema direct kama ndio lengo la sisi kwenda pale mama hakutaka kila mtu ajue shida zake na hakuwa mtu wa kupenda kuomba misaada sana (nadhani aliwahi kwenda pale kabla na kuona mabegi ambayo hayatumiki yapo pale so alijua kabisa hatokosa begi)

Nilifurahi sana kupata begi lenye nembo ya spots kama wenzangu hata uchovu wa kutembea uliisha wote.

Leo hii ndio nakumbuka kuwa mama alijitoa kwa ajili ya furaha yangu

Leo ndio naona kwa namna gani mama hakuwa na uwezo wa kunitunza

Leo ndio naona kuwa mama ni mama tu hata kama hana kitu

Leo nazidi kuona thamani ya mama ambae sina tena.

Natamani mama yangu arudi aone hatua ambazo mwanae nimepiga,

Mama hajawahi kula directly faida ya uzao wake kabisa

Mama hajawahi ona matunda wa mtoto wake kabisa

Ni kama alinizaa kwa lengo la kuteseka na mimi kisha kufa kabla hajafaidi matunda ya uzazi wake.

Kama una mama bado yupo hai

Kama una mama na umeweza kupata maisha kwa sasa

Kama una mama haijalishi yukoje,

Nakuomba mtunze sana mama yako

Kwa sababu mama uliyenae leo kuna siku hutokuwa nae tena.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kupata Kidogo Ni Bora Kuliko Kukosa Kabisa (Something Is Better Than Nothing)

Next Post

Kuna Wakati Maisha Ni Simulizi Isiyoelezeka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Epuka Kujinenea Mabaya

Weka mazoea ya kuwaza mambo Chanya kila mara Bila kujali maisha yako ya sasa wala vikwazo ulivyo navyo Kadiri…

Huruhusiwi ku copy makala hii.