
KAMA UNA SIMU JANJA (SMARTPHONE) NA UNASEMA HUNA MTAJI, JITAFAKARI UPYA!
Upo na simu janja pengine hata ya gharama kubwa
Una Elimu, ujuzi au kipaji fulani na hata uzoefu wowote
Au pengine una fahamiana na watu wengi wenye biashara zao!
Una uwezo wa kuweka vocha hata elfu 1000 tu kila siku
Lakini wakati huo huo unasema huna mtaji wala biashara au njia ya kukuingizia kipato!
Hakika shida sio mtaji wala kipato, shida ni wewe binafsi
Yani hata ukipata milioni 100 za mtaji bado zitapotea tu
Kwa ufupi tu ni kuwa kwa maisha ya sasa simu peke ake ni mtaji tosha
Huhitaji mtaji mwingine kuanza kupata kipato au kuanza biashara
Badala ya kutafuta mtaji mwingine geuza simu yako kama mtaji mkubwa
Jifunze kutumia simu kupata pesa badala ya kutumia kuingizia wengine faida na utajiri!
Acha kulalamika Huna mtaji wakati huo huo una shinda Instagram na tiktok kuangalia video zisizo kuingizia chochote.