
Kila siku kabla ya kulala tenga dakika chache tu jiulize, kama ikitokea Mungu amekuchukua muda huo, je utakuwa sawa na huna deni lolote kwenye maisha yako?
Kifo hakina muda maalumu wa kukufikia…
Kifo huja wakati wowote na mahala popote tena kwa mtu yoyote
Haijalishi kiwango cha pesa alicho nacho muhusika!
Wala haijalishi ukubwa wa nafasi ya uongozi wa mtu
Na hata haijalishi yule mtenda mema sana wala muovu sana
Pia hakichagui mtu mzima au mtoto mdogo
Kiufupi kifo hakina huruma kwa mtu yoyote yule!
Na mbaya zaidi wala hakitoi taarifa yoyote au kuonesha dalili za wazi kuwa kina karibia
Kuna watu ni wagonjwa mahututi na walitegemewa kufa wakati wowote Ila wapo hai mpaka sasa na wale wazima wamekufa
Kuna sababu nyingi za vifo, ukiondoa maradhi au ajali.. Kuna vile vifo vya ghafla tu mtu huzimika kama mshumaa!
Hivyo wakati unafurahia maisha yako na kutenda hile au lile, pia jiandae na kifo chako mapema
Wakati unatembea juu ya ardhi kwa maringo, unadhulumu na kuumiza wengine.. Kumbuka na kifo chako!
Tenga muda kila siku kabla ya kulala jiulize tu ikiwa utalala na kesho usiweze kuamka tena,
Umetengeneza mazingira mazuri kwa wategemezi wako na wewe binafsi huko uendapo?
Je, jasho lako ambalo linakutoka kila siku kwa ajili ya mali unazo tafuta… Zitabaki na kuwafikia watu sahihi unao watafutia?
Kuna wengi hutunza mali zao kwa siri sana hata wenza wao au ndugu wa karibu huwa hawana taarifa yoyote,
Baada ya kifo mali zote hupotea kama utani kisha wategemezi muhimu hubaki makapuku bila msaada wowote ule.
Kwahio kuanzia leo jitahidi sana kuandaa mazingira ya leo yako Ila usisahau kesho ambayo hutokuwepo
Tengeneza mazingira ya kifo chako kwa Mungu huko uendako lakini pia usisahu kuweka mazingira sawa kwenye mali unazotafuta
Ili hata ukizimika leo kama mshumaa basi angalau jasho lako libaki kwa watu sahihi unao teseka kwa ajili yao.
Kumbuka kitu pekee ambacho kila binaadam ana uhakika wa kukipata ni KIFO.