
Kuna vitu huwa havibadiliki haijalishi utatumia nguvu kiasi gani
Kuna mambo yakishatokea huwa yametokea
Kuna maamuzi yakishapitishwa huwa yamepitishwa
Na kuna watu wakishabadilika huwa wamebadilika
Sasa kuendelea kutaka mambo yawe tofauti kwa namna unayotaka wewe ni moja kati ya njia kuu ya kujiumiza wewe mwenyewe
Kuna muda njia pekee ya kupata nafuu ni kukubali UHALISIA
Usilazimishe nyekundu kuwa kijani mahala ambapo haiwezekani
Kukubali matokeo au uhalisia ni nusu ya kupata dawa na tiba
Acha kabisa kulazimisha mambo ambayo yameshindikana
Utamaliza pesa na muda wako bure mbaya zaidi utakosa raha na amani ya maisha
Kama jambo haliondoi uhai wako wala afya yako… Kubali uhalisia wake tu
Afya na uhai pekee ndio hazina kubwa zaidi ya maisha
Vitu vilivyobaki vyote vinaweza kupatikana wakati wowote
Haijalishi itachukua muda kiasi gani kuvipata tena!
Vile vile bila kujali ukubwa wa maumivu unayopitia au gharama ulizotumia.. Kubali Uhalisia
Pokea matokeo kwa mikono miwili kisha jiruhusu na jipe nafasi ya kupata vilivyo bora zaidi
Kila jambo hutokea kwa sababu maalumu kwenye maisha
Kwahio jifunze kutotaka mashindano yasiyo na msingi hata kwenye vitu vinavyotafutwa na kupatikana
Kubali Uhalisia wa mambo na utapata nafasi na fursa mpya pengine nzuri kuliko za mwanzo.