Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Kuna Wakati Maisha Ni Simulizi Isiyoelezeka

Kwenye pita pita zangu za mitandaoni nimekutana na video ya bibi mmoja kutoka Kenya anaesomasha wajuu zake kwa shida

Bibi ambae amepeleka kuku watatu shuleni (badala ya pesa taslimu ya ada) ili wajukuu zake waendelee kusoma!

Hilo tukio limenikumbusha mbali sana kuhusu maisha yangu pia na mama yangu

Nakumbuka niliwahi kuishiwa viatu vya shule (nilivyokuwa navyo vilitoboka kabisa ile sole ya chini hivo kisigino kikawa kinagusa mchanga kila nitembeapo)

Mama hakuwa na uwezo wa kununua kiatu kipya kabisa kutokana na ugumu wa maisha

Nilikuwa namuomba kila siku kuwa nataka kiatu kingine maana watoto wananicheka sana shuleni

Nilihisi mama hataki tu (akili za utoto) kumbe mama anaumia zaidi yangu ile hali.

Siku moja aliniambia tutaenda dukani kununua kiatu (eti kuna sehemu kaona wanauza viatu vizuri sana)

Ila tukiwa pale wakati anaongea na muuza duka kuhusu bei basi na mimi niingilie kati na niseme,

“Kaka nisaidie tu kwa pesa hii ayaliyonayo mama yangu ili na mimi nisome” 😭

Kumbe mama alishaenda mpaka duka la viatu na muuzaji alimtajia bei ya kiatu Ila mama hakuwa na uwezo yaani alikuwa na bei pungufu,

So mama alimuomba sana ila yule kaka alikataa kabisa, hivyo basi (aliamua kurudi kutafuta pesa zaidi ila bado haikufikia bei ya kiatu)

Ndio maana alitaka niende nae ili kuongeza uzito na kulainisha moyo wa yule kaka ili apokee kiasi ambacho mama amepata (alijua kabisa muuzaji hawezi pokea mpaka pesa itimie so aliona bora atumie njia ya kwenda na mimi).

Kweli bhana tulifanikiwa kupata kiatu kwa bei pungufu zaidi!

Unajua ilikuwaje (baada ya kufika pale na mama kuanza kuongea na muuzaji, bado aligoma kabisa hivyo mimi tayari nilikipenda kiatu baada ya kukiona ukizingatia nilikuwa na uhitaji sanaa)

Hii ilipelekea nianze kulia nilipoona muuzaji anamkatalia mama kupokea ile pesa (nilijua ntakosa kiatu hivyo nitarudi kutembea kwa kiatu cha zamani na kuchekwa)

Sikulia sababu ya kuigiza ili nipate kiatu, Ila nilijikuta nalia kwa uchungu sana wa kuona naenda tena kuchekwa na wenzangu

Unajua akili za utoto sikujua hata kama mama anaumia au anapitia shida zaidi yangu,

Mimi akili iliwaza kuchekwa na watoto shuleni, hii ikafanya nilie kwa uchungu sanaa, kwanza hata maneno ya mama kuhusu kumuomba muuzaji niliyasahu kabisa!

Hata kama wewe ndio muuza viatu katika hali kama hio nadhani ungelainika tu

Hata uwe na roho ngumu kiasi gani, ungepata huruma sana na kunipa hata bure.

Na hivyo ndivyo nilivyo pata kiatu kipya (mama alifurahia sana akijua nimeigiza vizuri zaidi ya alivyonifundisha kumbe mwenzake nilikuwa serious zaidi.

Maisha yana kila aina ya mitihani na kama unaona kabisa unaweza kumsaidia mtu muhitaji,

Kwa namna yoyote ile unayoona inafaa basi msaidie tu maana watu wana pitia magumu sana huwezi elewa kabisa mpaka yakufike.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kama Umefanikiwa Angalau Kidogo Na Una Mama Yupo Hai Basi Mtunze Sana Mama Yako

Next Post

Usijione Mjanja Sana Kupata Kabla Ya Wengine, Kumbuka Maisha Hayana Bajeti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Usiogope Kujaribu

Usiogope kujaribu jambo hata kama unahisi huliwezi au ni gumu sana Kataa kabisa neno haiwezekani kwenye akili…

Huruhusiwi ku copy makala hii.