Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Kupata Kidogo Ni Bora Kuliko Kukosa Kabisa (Something Is Better Than Nothing)

Nakumbuka mwaka ambao nilikosa mkopo wa Elimu ya juu

Hivyo kulazimika kurudi Dar es Salaam kuanza upya kutoka iringa

Kumbuka (niliuza vitu vyangu vya ndani ili kufanya maandalizi ya awali ya chuo na bado nikakosa mkopo)

Nilipofika Dar sikuwa na kitu chochote cha kuanzia hivyo kulazimika kutafuta kazi

Kazi ya kwanza ilikuwa usafi wa ofisi (pale banana AVIATION yaani mamlaka ya usafiri wa anga) nilipata kazi ya usafi kwa connection ya mama mmoja rafiki yangu (alikuwa ndugu wa mmiliki kwenye kampuni ya usafi)

Nilifanya kazi pale kwa wiki moja, changamoto kubwa ilikuwa mahala pa kuishi maana sikuwa na chumba pia sikutaka kabisa kukaa kwa ndugu yoyote na hata ndugu sikutaka wajue kama nimekosa mkopo na nimesha rudi dar (hawakuwa na msaada wowote ule zaidi wangezidi kunicheka)

Baada ya kuona sina mahala rasmi pakuishi, changamoto za usafiri pamoja na chakula +mshahara wa laki na nusu na bado nataka kutunza pesa ili mwaka utakaofata nirudi kusoma,

Niliona kabisa sitoweza ile kazi hivyo nikamuomba tena yule dada rafiki yangu anitafutie tena kazi nyingine ya ndani (housemaid)

Uzuri wa kazi ya ndani ni kula na kulala bure +uwezo wa kutunza pesa japokua nilipata kwa mshahara wa laki moja.

Sasa kuna dada mwingine ambae ni mdogo wa yule dada rafiki yangu aliyenitafutia kazi

Huyu binti alikuwa mrembo sana (mzuri mno kwa sura na umbo aise)

Hakuwa na kazi licha ya Degree ya ualimu aliyokuwa nayo miaka mitatu toka ahitimu masomo yake

Hivyo alikuwa anakaa kwa dada yake kwa matumaini ya kupata kazi serikalini (hakutaka kabisa kazi nje ya Elimu yake).

Baada ya kupata kazi yangu ya ndani, niliwaza kwanini yule dada asiende pale AVIATION kushika ile nafasi yangu niliyoiacha!

Kwanini anakubali kupoteza muda kusubiri ajira isiyo na matumaini?

Kwani atapungukiwa nini kufanya pale kazi angalau apate pesa za vocha?

Pia kwa uzuri wake alionao + Elimu yake atakutana na watu wengi wanaoweza kumshika mkono

Kumbuka ofisi ya mamlaka ya usafiri wa anga kuna mabosi wazito sana, wenye pesa zao na connection kubwa kubwa za maana tu

Mimi ningeweza kubaki shida ilikuwa sehemu ya kukaa (japo nilipata mtu wa kuishi nae Ila siwezi elezea zaidi maana kila mmoja anajua maisha ya dar na kuishi kwa mtu)

Niliamua kumshauri yule binti (tayari tulikuwa na mawasiliano)

Mwanzo alikataa sana na alisema hawezi fanya kazi za aina ile kabisa maana hana shida ndogo ndogo!

(pia alikuwa na kiji boyfriend wanacho danganyana)

Ila sikuacha kumpa ushauri kila siku mpaka ndani ya wiki moja hivi alikubali kufanya kazi (alisema nafanya kwa vile sitaki kukuvunja moyo Ila hii sio type yangu na ndani ya mwezi tu ntaacha)

Nilifurahi sanaa kuona nimeweza kumshawishi na kweli alienda kuanza kazi pale japo mwanzo aliona shida maana hajazoea kazi ngumu

Kila siku ilikuwa lazima anipigie simu eti anaacha kazi,

Niliendelea kumpa moyo kuwa ataozea tu ajikaze maana mwanzo huwa mgumu sana.

Guess what baada ya kupata mshahara wa kwanza hakuacha kazi, alizoea na kuacha kulalamika

Alipata marafiki wapya bila kusahau sponsor wa kumbustisha maisha (sio jambo zuri Ila kwa mazingira yale asingeweza kumkataa mtu anae mpa maisha zaidi)

So maisha yakawa laini kwake, alipendeza akabadilika na mwisho alihama kwa dada yake na kwenda kujitegemea!

Baada ya mwaka yule sponsor alimpa connection ya kazi (kigamboni kwenye zile kampuni za mafuta na gas)

Yes mjini hapa connection ndio kila kitu na mpaka sasa yule dada ana maisha mazuri siwezi kusema kwa kiwango gani Ila haachi kunishukuru.

Jiulize angeendelea kukaa kwa dada yake kusubiri ajira za CCM angepata lini?

Angeendelea kulala ndani, saa ngapi angekutana na sponsor?

Angetoa wapi connection ya kazi ambayo kwa sasa inamlipa zaidi ya mshahara wa Ualimu?

So siku zote ni bora kutoka kutafuta upate chochote kuliko kukaa ndani

Bora utoke uonekane nje hii itakusogeza karibu na bahati nasibu kuliko kukata tamaa ukiwa ndani

Toka fanya kazi yoyote nje huku ukiendela kungoja kazi nzuri zaidi unayotamani

Jichanganye mahala popote unapopata riziki usijione cake sana kisa uzuri na Elimu yako

Muda haukusubiri na mafanikio huenda kwa anaeyatafuta.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Mteja Ni Mfalme, Mpe Heshima Yake

Next Post

Kama Umefanikiwa Angalau Kidogo Na Una Mama Yupo Hai Basi Mtunze Sana Mama Yako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Jifunze Kushukuru

Kadiri unavyo shukuru Ndivyo unavyojisogeza karibu na mafanikio yako Jifunze kuwa na moyo wa kuyaona mazuri…

Huruhusiwi ku copy makala hii.