Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Kuwa Na Afya Ya Akili Nzuri Ni Muhimu Sana Kuliko Mafanikio Ya Fedha

Kulinda afya ya akili binafsi ni kitu muhimu sana kwenye maisha

Asilimia kubwa sana ya maisha tunayo ishi hususani nchini Tanzania ni chanzo kikubwa cha afya ya akili Kutokuwa sawa

Watu wengi wanapitia changamoto ngumu bila wao kujua

Aina ya maisha na mazingira kwa asilimia kubwa Tanzania ni magumu sana kiasi kwamba hufanya akili kuvurugika mara kwa mara

Watu wamejaa visirani na makasiriko ya hapa na pale

Kila mmoja anaishi kwa machale muda wote bila kujiamini

Ugumu wa maisha na matatizo ya kila aina pia ni chanzo cha akili kweda resii sana

Hata upatikanaji wa huduma mbali mbali ni katika namna ngumu inayopelekea akili za watu wengi kukosa utulivu

Kwa hakika ili akili ipate wakati mzuri wa kufikiri na kugundua mambo mengi, utulivu ni jambo la msingi zaidi

Wengi wanaishi maisha magumu sana ukiachilia ugumu wa kipato, bila wao wenyewe kujua

Tanzania hata ujitahidi kwa kiwango gani kuweka akili sawa bado kuna namna utashindwa,

Kutokana na mtindo wa maisha ya watu kila siku

Vile vile mtindo wa maisha ulio andaliwa na viongozi wanaoshikilia nchi

Hakika watu wanateseka sana hata bila wao kujua kama wanapitia mateso

Kila kitu kupata ni shida na mlolongo mrefu sana licha yakuwa haki kwa mtu

Kuna watu wengi sana wakubwa kiumri hata ki cheo na mafanikio Ila mambo wanayofanya ni kama watoto wadogo!

Matendo na maneno yao hayaendani kabisa na umri au cheo katika jamii zao

Hakika ni msiba mzito sana kwa wakazi wa nchi yetu kwa ujumla

Hii ndio zaidi inapelekea mmomonyoko wa maadili kuzidi kukithiri maana hata hao waliopewa dhamana ya kuweka sawa maadili wanaona sawa tu kwasababu na wao afya zao za akili zinaona sawa

Kila mmoja ana pambana kuziba njaa ya tumbo lake bila kujali mangapi yana haribika!

Njia kubwa zaidi ya kusaidia kuishi na kuweka akili sawa ni pamoja na kuchukulia kila kitu katika namna chanya

Kutofatilia kila jambo linalotokea hasa kama ni nje ya malengo yako

Bila kusahau kujiweka mbali na mazingira au mtu yoyote ambae ni sababu ya kuharibu akili yako

Kufanya tahajudi mara kwa mara na kutafuta muda wa peke yako

Kufuatilia vitu vichache vinavyojenga na kuboresha uwezo wa kufikiri

Bila kusahau kusoma sana vitabu na kusikiliza podcast mara kwa kwa mara

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kufa Na Tai Shingoni Kwenye Baadhi Ya Shida Zako

Next Post

Usimsaidie Mtu Msaada Ulioficha Manyanyaso Kwa Ndani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.