
Usiumizwe sana na wanao tangulia kupata kabla yako
Usipate presha kuona wengine wametangulia zaidi yako
Usilie sana kuona wengine wanapiga hatua za mafanikio kuliko wewe
Usijidharau au kujiona mnyonge sababu ya wengine wanaokuzidi kwenye maisha
Usikimbizane na wengine kwa kuhisi unaachwa nyuma zaidi
Usimlaumu Mungu na kudhani anakuacha kwa makusudi
Usifanye mambo mabaya na maovu kisa haraka ya kutaka kuwa kama wengine
Usikimbilie mahala ambapo maisha bado hayaja kupeleka
Kuwa na subra, Hakika kila mmoja hupata kwa muda wake sahihi
Hakuna anae wahi sana wala anaechelewa sana hapa Duniani
Hakuna mjanja sana wala mjinga sana kwenye muda wa kufanikiwa
Kupata mapema sio tiketi ya kudumu nacho milele
Wapo waliotangulia kupata na sasa hawana tena
Na wapo waliochelewa kupata na bado wanavimiliki
Ikiwa unafanya unayopaswa kufanya katika njia zako
Unajituma na kupambania hatma ya maisha yako
Unatafuta fursa kwa nguvu na akili zako
Unafanya juu chini kuboresha maisha na kutimiza malengo yako
Basi inatosha sana na huna haja ya kuumia kwa sababu ya wengine walio mbele yako
Heshimu sana mapambano yako na kuna siku utapata kwa muda na wakati sahihi.