
Kama unataka mabadiliko kutoka kwa wengine basi anza kubadilika wewe
Ikiwa unatamani wengine wafanye yale unayotaka basi anza kuonesha mfano
Endapo unaona jambo fulani linafaa kufuatwa na lina faida kwa watu basi anza wewe kabla yao
Haijalishi unataka mabadiliko eneo gani, Ila kama yanahusisha watu wengine elewa kuwa unapaswa kuwa mfano kwa kwanza
Inawezekana umechoka tabia fulani za watu juu yako na unataka wabadilike, anza wewe kubadilika
Au pengine kuna namna unahisi wengine wanapaswa kuishi kwa namna unayoona ni sawa, anza wewe kuonesha mfano
Huwezi badili tabia ya mtu mwingine ikiwa bado unaishi kama yeye!
Huwezi lazimisha mabadiliko kwa wengine ikiwa bado unaishi maisha yale yale uliyo zoeleka
Kama umechoka kudharauliwa, kuna uwezekano mkubwa wewe ndio chanzo cha watu kukudharau, hivyo anza kujithamini kwanza
Badilika wewe kwanza, badili mfumo wa maisha yako, badili tabia zako kisha wengine watafuata nyayo zako!
Ukiona eneo lolote lina shida na una husika nalo kwa namna moja au nyingine, jikague wewe kwanza kabla ya kukagua wengine!
Huwezi badili mtu mmoja, jamii au Dunia nzima ikiwa wewe bado unaishi katika mifumo ile ile
Badilika wewe kwanza kisha acha waamue kubadilika au kubaki vile vile na hilo halitokuwa jukumu lako tena.