
Hakuna namna yoyote ile kwamba ukiwa kwenye mahusiano na mtu mwenye mafanikio na wewe utapata
Hakuna muujiza wa kuwa kwenye mahusiano na tajiri kisha na wewe akakuambukiza utajiri wake
Hakuna jinsi yoyote ya kuwa na mtu mzito sana au mkubwa sana au kiongozi wa juu sana halafu na wewe akakuambukiza ukubwa na uzito wake kwa njia ya ngono
Kuna watu wengi walioana na watu wenye mafanikio makubwa mno Ila wakaachika au kutengana wakiwa makapuku kama walivyo enda
Kuna wengine walipoteza wenza wao waliokuwa na mafanikio makubwa sana na wakabaki mafukara baada ya muda mfupi sana
Kuna wale walikuwa au wapo na wenza wenye pesa nyingi sana mpaka sasa lakini hawana kitu chochote wanacho miliki wao binafsi
Bila kusahau wapo wanao pewa kila kitu hata mitaji mikubwa na wenza wao na bado hupoteza yote!
Ijapokuwa wapo walio bahatisha kupata mafanikio makubwa kupitia mwenza wao bila jitahida kubwa sana za pembeni, ambapo ni kama kucheza kamari na kusubiri bahati nasibu au usafiri wa meli Airport.
Kuwa na tajiri kwenye mahusiano ni jambo moja na kutajirika kupitia yeye ni jambo la pili
Mafanikio ni pamoja na matumizi sahihi ya akili, jitihada na mchakato wa aina fulani tukiondoa uwezo wa kuwa na pesa za kufanyia kitu!
Kuwa na mtu mwenye mafanikio ni moja kati ya njia inayo ongeza uwezekano wa kufanikiwa…..
Wakati huo huo jitihada za akili za pembeni zikihitajika.
Kupoteza muda kuwa na tajiri au kunyanyasika kisa upo na tajiri kwa matarajio ya kuwa tajiri huku huna mkakati wowote wa ziada ni moja kati ya kujikosea heshima na haki zako za msingi hapa Duniani
Ukiamua kuwa na tajiri kwa sababu zingine ni sawa Ila usitarajie kuambukizwa utajiri wake kimiujiza nje ya jitihada zako binafsi.