
Wakati unasema hakuna mapenzi ya kweli, kuna watu wanafunga ndoa kila siku
Wakati unasema biashara ngumu, kuna watu wana fungua biashara mpya kila siku
Wakati unasema hakuna ajira, kuna watu wanaajiriwa kila siku! Na kuna kampuni zinatangaza kazi kila kukicha
Wakati una fikiria kuhama nchi au mkoa fulani kuna watu wanapigania kuhamia ulipo kila siku kwa uwepo wa fursa ambazo wewe hujaziona!
Wakati unasema utaanza kesho, kuna wenzako wanakesha kufanya kitu hiko hiko kila siku!
Wakati unasema maisha magumu, kuna wale wanaokesha wakitumia pesa kila siku!
Kila unaposema ukiwa na kitu fulani ndio utafurahi kuna watu hawana chochote na wana furaha ya kweli ndani yao
Kila unaposema biashara fulani hailipi kuna watu wanafanya biashara hio hio miaka kibao na wanaendesha maisha yao.
Kimsingi hakuna kitu kibaya, kigumu wala kisichowezekana
Yote hutegemea upande wako wa akili ulipoelekea
Ukiamua kuona ugumu Hakika itakuwa zaidi ya ugumu na ukiamua kuona wepesi bila shaka utapata njia ya kufanya unachotaka…
Maisha sio kombolela japo wapo wanao butua..
Maisha sio bahati Ila wapo wanao bahatisha..
Maisha sio mateso lakini wapo wanao teseka!
Maisha ni uchaguzi wa matumizi ya akili kwa mtu binafsi,
Kila mmoja hufanya maamuzi yeye mwenyewe ya kuitawala akili yake na akili huamua kumzawadia kile kinachomfaa.