Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Maumivu Ya Kiatu Cha Juma, Anayajua Juma Mwenyewe

Mwisho wa siku maumivu uliyonayo, shida unazopitia, matatizo yanayokuzonga na hata uzito wa changamoto zako zote hubaki kwako wewe mwenyewe

Haijalishi utapewa Pole na watu wangapi, wala haijalishi utagusa mioyo ya watu wangapi!

Kamwe watu hao hawawezi kuvaa wala kubeba uzito wa jambo lako kwa kiwango ambacho wewe binafsi umebeba.

Hivyo kwenye maisha yako kaa ukijua kuwa unajihitaji wewe kwanza kabla ya mtu mwingine yoyote,

Elewa kuwa maisha yako yanaanza na wewe lakini pia yanamaliza na wewe mwenyewe.

Unapaswa kuvaa uhusika wa maisha uliyonayo kwa kila hatua na kila sekunde kwa maana wewe ndio star wa movie unayocheza!

Anza na wewe kisha maliza na wewe kwa maana kuwa…

Jioone huruma kabla hujataka kuonewa huruma na wengine,

Jipongeze wewe mwenyewe kabla hujataka pongezi kutoka kwa watu wengine,

Jikumbatie wewe binafsi kabla hujataka kumbato kutoka kwa mtu mwingine

Lakini pia jililie na jinenee mema wewe mwenyewe kabla hujanenewa na watu wengine,

Pia usisahu kujipa umuhimu wewe kwanza kabla hujalilia kupewa umuhimu kwenye maisha ya watu wengine

Na usisahu kujipa pole wewe kwanza kabla hujapewa na mtu mwingine yoyote yule bila kujali uhusiano wako wewe na yeye.

Unapaswa kuelewa kuwa kila mmoja ana viatu vyake kwenye mguu wake binafsi

Huwezi kujua kwa namna gani kiatu cha mwingine hupwaya au kubana mguuni kwake kamwe kwakuwa viatu vile hujavaa wewe,

Hivyo hivyo wengine hawawezi elewa kiasi gani kiatu ulichovaa kinabana au kupwaya mguu wako!

Hivyo basi uzito wa mapito na maumivu ya kiatu chako unayajua wewe mwenyewe binafsi,

Na kamwe huwezi ambukiza maumivu yako kwa watu wengine kama ambavyo hawawezi kuambukiza maumivu yao kwako!

Simama wewe na wewe mwenyewe kwanza kabla hujataka wengine kusimama na wewe.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kuna Watu Wapo Kama Maharage, Kadiri Yanavyoruka Ndivyo Yanavyoiva

Next Post

Kuna Wakati Unapaswa Kuacha Inyeshe Ili Ujue Panapovuja!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Jifunze Kushukuru

Kadiri unavyo shukuru Ndivyo unavyojisogeza karibu na mafanikio yako Jifunze kuwa na moyo wa kuyaona mazuri…

Huruhusiwi ku copy makala hii.