Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Mteja Ni Mfalme, Mpe Heshima Yake

Mteja hanuniwi, hatukanwi wala kusemwa kwa ukali hata kama amekosea au kukuudhi sana,

Mteja hunyenyekewa na kupewa thamani kubwa sana kwenye biashara yoyote unayofanya.

Mteja ni zaidi ya mfamle anapaswa kuhudumiwa na kusikilizwa vyema!

Mteja ndiye ameshikilia uhai wa biashara yako unayofanya anaweza kuiua au kuihuisha wakati wowote!

Mteja ndiye alikufanya uanzishe, uendeshe au usimamishe biashara yako!

Kila uamkapo asubuhi na kwenda kufungua biashara, sababu kubwa ni mteja au tuseme wateja kwa lugha ya wingi

Hivyo mteja wako anapaswa kulindwa kwa gharama yoyote haijalishi ukubwa wa kitu anacho nunua kwako.

Kama ameweza kuacha biashara za wengine kisha kuja kununua kwako, basi anasababu zake za msingi ambazo unapaswa kuzizingatia ili asiende au kupata chaguo lingine nje ya biashara yako.

Hupaswi kumpa mteja akili ya kuwaza au kufikiria chaguo lingine nje ya huduma au bidhaa zako!

Haijalishi mteja huyo yukoje, Thamani yake inapaswa kubaki vile vile hata kama anakuja mara moja moja au ni mteja wa kila siku na mzoefu.

Haijalishi amenunua kitu cha gharama ndogo sana au kubwa sana

Wala haijalishi tabia na mwenendo wake nje ya biashara yako.

Kitu cha msingi unachopaswa kuzingatia ni kumjali na kumlinda mteja wako kwa namna yoyote ile hata kama ndio siku ya kwanza kuja kwenye kununua kwako!

Mteja anapaswa kufurahishwa na kupewa mapenzi ya dhati kwenye biashara hata zaidi ya yale unayo wapa uwapendao!

Mteja hupaswa kupewa heshima kubwa sana nje au hata ndani ya biashara unayofanya,

Ukimjali na kumthamini mteja wako, basi na yeye atajali na kuthamini manunuzi ya huduma au bidhaa zako.

Kitu pekee ambacho unapaswa kuzingatia zaidi ni kuhakikisha pesa ya mteja inakuja kwenye biashara yako mara kwa mara, tena na tena au zaidi na zaidi.

Hata akinuna, akiwa na tabia mbovu, akikusema vibaya nk hayo yote hayapaswi kuzingatiwa ikiwa analeta pesa kwenye biashara unayofanya.

Zingatia na mjali mteja wako ili alete wateja zaidi kupitia furaha na namna anavyoridhika kununua kwako.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Huhitaji Kuwa Bora Na Mkalimilifu Ili Kuanza, Anza Hivyo Hivyo Ulivyo

Next Post

Kupata Kidogo Ni Bora Kuliko Kukosa Kabisa (Something Is Better Than Nothing)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Usiogope Kujaribu

Usiogope kujaribu jambo hata kama unahisi huliwezi au ni gumu sana Kataa kabisa neno haiwezekani kwenye akili…

Huruhusiwi ku copy makala hii.