
Haijalishi una sababu kubwa zaidi za kuacha na kukata tamaa
Haijalishi una vikwazo visivyopingika na changamoto za wazi
Hata kama sababu zingine umezaliwa nazo au hata umezipata bila kukusudia kabisa
Kuna zile sababu za kimaumbile au hata za kiuumbwaji..
Maisha yataendelea mbele hata kama una sababu za kukata tamaa zaidi ya 100…
Siku zitasonga, dakika zitaisha, miezi itaenda na hata miaka itakata
Kama hautobadilika ukweli ni kuwa maisha yataendelea na wewe ndio utabaki vile vile!
Maisha hayana huruma na mtu yoyote bila kujali mateso yako nyuma ya pazia
Wala maisha hayatakupa nafasi ya pili kurekebisha muda uliopoteza
Muda ukipotea elewa kuwa hakuna namna yoyote ya kuurudisha nyuma tena
Hivyo bila kujali mangapi umepitia wala sababu gani inakufanya ukate tamaa,
Acha kulia, inuka na jipe moyo wa kusonga mbele kwa mara nyingine
Hakuna muujiza wa muda kurudi nyuma, hakuna dawa ya muda kurudi nyuma wala maombi yatakayo rudisha muda wako nyuma!
Ni lazima ujiinuue, ujivute, ujikokote ikibidi hata ujiburuze kwenda mbele wewe mwenyewe kwa jitihada zako.
Jipe moyo, jishauri, jitafutie njia na suluhisho la changamoto zako kwa lengo la kusonga mbele tu
Bila kujali ukubwa au udogo wa hatua zako, wala ukubwa au udogo wa mabadiliko unayofanya..
Jambo la msingi ni kubadilika na kwenda mbele tu
Hata kama utatumia miaka mingi kufika, ikiwa unafanya kitu sahihi ndani ya muda sahihi kwa njia sahihi,
Hakika UTAFIKA NA KUFIKIA UNACHOTAKA! Na endapo utakosa hakika huwezi kuwa sawa na ulivyokuwa awali.