
Mungu hajaumba viumbe wake hususani binaadamu,
Kwa uwezo mkubwa sana kisha binaadamu huyo huyo aje kuzurura kisha kufa
Mungu ameumba binaadamu kwa maarifa mengi sana sio kwa lengo la binaadamu huyo kuzurura na kufa
Furaha ya mungu sio binaadamu wake kuwa mzururaji haijalishi ataishi kwa miaka mingapi Duniani
Tukiondoa wale ambao hufa mapema kabla ya umri wa kujiambua,
Wengine wote wanapaswa kufanya kitu kwa ajili ya Mungu wao!
Kama una miaka zaidi ya 18 sasa una afya njema na huna ulemavu mkubwa wowote basi tambua una deni kwa aliyekuumba.
Uliwashinda ndugu zako wengi wakati mbegu yako ikikimbia kulitafuta yai la mama ndani ya via vya uzazi
Maana yake uliweka mkataba na Mungu kuwa wewe ni bora kuliko wengine na ukapewa nafasi ya kuumbwa
Wengine wote wakatolewa nje kama uchafu na wewe kama kiumbe
Sasa kwanini bado una kubali kuwa mzururaji?
Kwanini una kubali kupoteza muda kulala ndani kwako?
Kwanini hutaki kabisa kufikirisha akili yako?
Kwanini unaleta uvivu usio na maana wakati una uwezo wa kubadili historia yako?
Kwanini bado una kesha nyumba za ibada kuomba msaada kwa Mungu wakati tayari amekuumba na kila kitu?
Abudu kwa kushukuru na kumtukuza Mungu sio kila siku kulilia shida ambazo hazina mantiki
Kuna watu wana kila sababu za kumlilia Mungu wao Ila sio wewe!
Shtuka usingizini pambania hatma yako kwanza
Muoneshe Mungu upo tayari kusimama na kumtukuza kwa vitendo
Vitendo vya upambanaji na nia ya kujikwamua kwa vitendo halisi
Kisha Mungu ataweka mkono wake katika jitihada zako.
Mfanye Mungu ajisifie kwa kile alichokiumba kupitia maarifa unayotumia Duniani
Mfanye Mungu afurahie na oene matunda ya uumbaji wake
Mfanye na yeye aseme Hakika sikupoteza muda kuleta kiumbe wa mfano wangu.
Sasa kiumbe wa mfano wa Mungu nae anakesha kumlilia Mungu ampe mkate wa siku pasi na jitihada zozote! Hakika ni maajubu makubwa sana ya Dunia.