Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Sikiliza Sauti Yako Ya Ndani, Ina Nguvu Na Imebeba Picha Halisi

Enzi za uhai wa Baba yangu alipenda sana starehe kama walivyo watu wengine

Baba alikuwa na kazi nzuri kiasi ambayo ilimtosha kwa mahitaji muhimu yote

Hakutaka kabisa kujenga nyumba ya kuishi, licha ya kuwa na mke tayari (stori hii alinisimulia mama)

Kati ya vitu ambayo Baba hakutaka kabisa, ilikuwa kumiliki nyuma ya kuishi

Uwezo alikuwa nao Ila moyo wake haukuwa tayari kwa hilo

Wengi walimshangaa sana kiasi Rafiki yake wa karibu aliamua kumshauri zaidi

Alimsisitiza mno faida za kujenga ukizingatia tayari ana mke na baba wa mtoto mmoja ambae alikuwa kaka yangu (kabla sijazaliwa mimi)

Hivyo kwa unyonge sana baada ya miaka mingine kupita, Baba angu aliamua kujenga nyumba yake maeneo ya Yombo Dovya Dar es Salaam

Hakujenga kwa sababu za mapenzi yake bali ushauri na msisitizo wa rafiki wa karibu sana na ndugu.

Mama na Baba walitengana miaka miwili baada ya kuzaliwa kwangu.

Na mama alirudi kigoma kwao akiwa na sisi watoto wake Ila baba alibaki Dar es Salaam kuendelea na maisha yake.

Baada ya Baba kufariki tena pengine hata hakufaidi sana ile nyumba yake maana aliijenga miaka michache tu kabla ya uhai kuondoka

Ilipita miaka kadhaa mingine na kaka kuwa kijana anaewaza kuhusu maisha na utafutaji kwa ujumla

Kaka yangu alitaka kuuza nyumba! Kama sehemu ya kupata mtaji wa kuanza biashara

Ila mama aligoma kabisa kuhusu suala la
nyumba kuuzwa akiamini kuwa itatusaidia baadae

Kaka hakutaka kabisa kusikia na aligombana mno na mama kisa kuuza ile nyumba!

Lakini mama alimzidi nguvu hali hio ilifanya angalau kaka kupunguza kelele kiasi

Miezi michache sana baada ya Mama kufariki pia, Nyumba iliuzwa!

Tena kwa bei ya hasara sana bila hata ya mimi kushirikishwa nikiwa kama mtoto na muhusika halali wa nyumba ile!

Nyumba iliuzwa kwa bei ambayo hata kiwanja chake tu ni zaidi ya bei ile!

Yani bei ya hasara sana kama vile kulikuwa na tatizo kubwa linahitaji pesa za haraka!

Nilipata maumivu makali sana baada ya kupata habari ile,

Ila sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo tu kwa sababu tayari maamuzi yameshapita!

Zile pesa ziliisha na kupoteza kama kimbunga! Hakuna kitu cha maana chochote kilifanyika na ikahesabika kama hasara kwa marehemu Baba.

Kuanzia hapo na mpaka sasa nilijifunza kitu kikubwa sana maishani

Sio kama Baba hakutaka kujenga, Ila pengine sauti yake ya ndani ilimuonesha kitu cha baadae

Pengine sauti yake ya ndani ilimuonya na kutaka afaidi pesa zake ujanani kwake au kwenye uhai wake

Pengine sauti ya ndani ilijua nini kitatokea baadae na alipaswa kuamini hilo kama lilivyo

Ila ushawishi na nguvu za watu wengine ulifanya apotezee kabisa sauti ya ndani yake kisha kupata hasara akiwa hayupo Duniani.

Simaanishi kuwa usijenge nyumba au kuwekeza kwa uoga wa kufa, bali unapaswa kuamini sana ile sauti ndogo ya ndani inayokusisitiza kuhusu kitu fulani

Maamuzi yoyote utakayofanya kupitia sauti yako ya ndani,

Yanaweza kupendwa na watu wengine na kuna wengine wakaona kama huna akili au umechanganyikwa..

Elewa kuwa hilo halihusiani na maisha yako kabisa na lisikuumize kichwa

KUNA MUDA UNAPASWA KUSIKILIZA SAUTI YAKO YA NDANI HASA ILE INAYOJIRUDIA MARA KWA MARA KWAKUWA INA NGUVU KUBWA KULIKO UNAVYODHANI.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kuteseka Sana Leo, Sio Tiketi Ya Kufurahia Maisha Ya Kesho

Next Post

Huwezi Kukamata Vipepeo Kwa kukimbizana Navyo, Tengeneza Bustani Nzuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Tengeneza Mabawa Yako

Usikubali mazingira yakwamishe ndoto zako wala kukupa vikwazo vya kuwa unavyojiona kwa ndani Usikubali watu…

Huruhusiwi ku copy makala hii.