Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Simama Na Hatma Yako, Kwakuwa Hata Waliofanikiwa Waliamua Kusimama Na Hatma zao

Mmoja kati ya rafiki zangu wa karibu sana enzi na enzi (anajua hustle zangu za mtaa maana tumepambana sana pamoja)

Aliwahi kuniambia “hivi mwajuma kwanini unateseka wakati una ndugu wenye uwezo mkubwa?”

Nenda kwa ndugu zako na jishushe wakusaidie kwanza, unapata shida za bure mama yangu.

Nilikuwa nimeshika kipande cha mkate muda huo nakula huku nashushia na maji ya kandoro (hapo mkate wenyewe kanipa yeye😁)

Huyu dada anaitwa Maria rafiki ambae alinipenda sanaaa unajua ile una rafiki anakupenda mpaka unajua kabisa licha ya kuwa sina hata mia (kuna huyu na mwingine anaitwa Gwamaka)

Maria alikuwa muuza duka la mchaga mmoja pale Tandika maguruwe ambapo nilikuwa naishi mitaa ile ile ya karibu

So nilijuana nae na kuzoeana nae sana maana maisha yetu ni kama yalifanana tu, japokuwa yeye alikuwa anauza duka na mimi nauza mama ntilie huku nasoma (nilisoma elimu ile ya kidato cha 5 na 6 kwa mwaka mmoja ile ya watu wazima mitaani tu).

Siku hio nilikuwa nimetoka shule usiku mida ya kama saa 2 hivi nimechoka hoi, miguu imejaa vumbi kali kwa sababu ya kutembea umbali mrefu (kutoka buguruni rozana kuna shule inaitwa Hekima uplands academic centre ) ndio nilikuwa nasoma pale,

Sikuwa napanda gari sababu ya kukosa nauli so nilishazoeaga kwenda na kurudi kwa mguu tu

Mara nyingi Maria alikuwa ananipa mkate na maji pale dukani bure kabisa (aise yule dada mungu ampe maisha marefu sana)

Sasa siku ile alionea huruma sana ndio kuanza kunishawishi niende kwa ndugu zangu na nijishushe wanisaidie maana wana uwezo huo,

Ni kweli kabisa nina ndugu wenye uwezo na ambao hawana uwezo pia.

Babu yangu mzaa mama yangu kigoma ana nyumba kubwa sana ya Ghorofa (kwa wenyeji wa kigoma wanapajua pale buzebazeba ujiji kituo cha darajani, kwanza ukiwa kigoma ujiji babu ni maarufu sana kutokana na ile nyumba maana hakuna nyumba kama ile maeneo yote ya pale)

Ukija kwa babu yangu mdogo (babu huyu na babu yangu mzaa baba ni mtu na kaka yake) nae alikuwa maarufu sana japo ameshafariki na alinilea sana, (so kwa wakati ule Maria alimaanisha nirudi kigoma kwa watoto wa babu yangu ambao awali walinitesaga sana)

Babu alikuwa na maisha mazuri mno na maarufu sanaaaaa kigoma nzima (alikuwa Mganga wa kienyeji Ila mwenye pesa zake)

Bado nina mama mkubwa (dada wa mama yangu kabisa) yupo dar es Salaam na ana mume wake maarufu sana Tanzania ni shekhe mkubwa sana na wengi wanamfahamu sana tu Ila ndio matendo yake na maneno yake haviendani.

Kwahio hao ni baadhi tu ya ndugu ninaoweza kusema nilipaswa kuwa chini yao Ila haikuwa hivyo!

Bado ndugu zangu wengine wengi sana wanamaisha mazuri mno kiuchumi siwezi kutaja wote (wengine wapo kigoma na wengine dar es Salaam).

So Maria aliongea na nilimuelewa sana maneno yake,

Nilimjibu hivi “NIMELETWA DUNIANI KUPAMBANIA HATMA YANGU, MPAKA SASA SINA SABABU KUBWA YA KUWA OMBA OMBA NA NINAPASWA KUSIMAMA MWENYEWE KUINUA MAISHA YANGU KAMA HAO NDUGU ZANGU WALIVYOINUA MAISHA YAO”

Ni kweli hakuna ambae hataki msaada Ila nadhani nipo tofauti kidogo

Nina amini kuwa kwa umri wangu wakati ule na changamoto za kuondokewa na wazazi basi ndugu walipaswa kupeana jukumu la kuhakikisha siadhiriki!

Ila hao hao ndugu licha ya uwezo wao, sikuona jitihada zao zozote (akufukuzae hakuambii toka, niliona tu naonekana mzigo kwenye maisha yao)

Hivyo nilikubali kupambana na maisha yangu binafsi kwakua…

Sikuwa kipofu, kilema wala mgonjwa kwa maana sikuwa na ulazima wa kusaidiwa.

Maria alikaa kimya tu Ila najua hakunielewa kabisa na alihisi kama nataka kupata kichaa cha maisha.

Umeletwa Dunia kusimamia maisha yako na sio kuwa mzigo kwa wengine

Kama huumwi ugonjwa wowote mkubwa

Kama huna ulemavu mkubwa wowote ule

Basi unapaswa kusimama na kuishi kwenye maisha yako

Haijalishi utateseka kiasi gani, tambua kuwa hata hao unaodhani wamefanikiwa sana pia waliteseka kupata hayo mafanikio.

Sina chuki na ndugu yoyote yule eti kwakuwa hawakunipa sapoti kwa maana najua kuwa kila mmoja anapaswa kusimama na uzao wake binafsi.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Usijione Mjanja Sana Kupata Kabla Ya Wengine, Kumbuka Maisha Hayana Bajeti

Next Post

Urafiki Wa Kweli Hauna Mashaka Wala Kipimo Cha Upendo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.