
Kuna vitu hupaswi kutumia nguvu kujieleza sana kwa mtu
Yapo mambo hayafai kabisa kutolewa maelezo ya ziada ili yaaminike
Kuna matukio hata hayapaswi kutolewa sababu za kwanini yanafanyika au yalifanyika
Halafu zipo nyakati huhitajiki kufungua mdomo wako kabisa zaidi ya vitendo tu, jibu moja au maneno machache tu
Ukijiona bado unajieleza sana kwa watu kisa kitu fulani…
Ukijiona bado unapaswa kutoa maelezo mengi ya kujitetea…
Kama upo kwenye kundi la kuhitajika ushahidi au shuhuda ili uaminike…
Tambua bado hujaanza KUISHI
Na mbaya zaidi hayo hayo maelezo unayotoa ndio chanzo cha kudharaulika zaidi.
Kwenye Haya maisha haijalishi utawaeleza watu mambo mangapi ya kweli au uongo
Kama mtu kaamua kuona kitu fulani ni bluu hata kama ni nyekundu, elewa kamwe huwezi badili akili yake
Kuna mtu akisha amini kitu hata kama alisikia uvumi bila uhakika basi tayari humtoi kwenye imani yake
Kuna mtu atajifanya anataka kujua ukweli kumbe pembeni ana ku ng’ong’a
Kuna mtu hutaka maelezo lakini kwenye akili yake tayari ameshafanya maamuzi mengine
Sio kila mtu anapaswa kukulia muda wako wa maelezo
Usipoteze muda na nguvu kutoa maelezo ambayo mwisho wa siku hayata badili chochote!
Toa maelezo sehemu kwa lengo la kujenga kitu bora zaidi
Jieleze pale penye faida na panapo lenga kukuingizia zaidi
Mengine yote ambayo hayana maana kwako wala kwenye maisha yako hayapaswi kukuchukulia muda wako wa maelezo
Acha waelewe kwa namna wanayotaka kuelewa
Acha waamini wa nachotaka kuamini
Ikiwa hakuna madhara ya moja kwa moja yatajitokeza kwako!
Mwisho wa siku muda sahihi ukifika ukweli hujitenga na uongo hujitenga hivyo acha muda uongee,
Kujenga heshima yako binafsi ni pamoja na kupunguza kujieleza sana au kutoa sababu kila wakati.