
Sio kila mlango unao uona mbele yako kwa macho ya nje umefungwa basi pia umelokiwa kwa funguo!
Kuna Milango imeegeshwa tu lakini kitasa kipo wazi
Kuna Milango ina vitasa vibovu kabisa au hata upo kwenye marekebisho
Kuna Milango imesahulika kufungwa na wahusika kwa bahati mbaya
Kuna Milango haifungwagi kabisa kwa funguo kutokana na sababu mbali mbali
Kuna Milango asili yake migumu tu mpaka utumie nguvu kufungua lakini haina loki yoyote
Ipo milango inatumia funguo Sawa na funguo uliyonayo wewe mwenyewe
Kuna ile Milango imejifunga sababu ya upepo tu lakini haina loki yoyote
Hivyo kabla hujasema huwezi kuingia ndani … Shika kitasa kwanza
Shika kitasa kwa nguvu na tumia uwezo wako wote kusukuma mlango ulio mbele yako…
Kama hautofunguka angalau unaweza kuwa na sababu ya kusema umeshindwa kuingia ndani!
Hivyo hata kwenye maisha yako kuna fursa zinakupita kutokana na mtazamo wa nje tu,
Kumbe ndani ya fursa hio kila kitu kipo wazi kina kungoja wewe!
Badili mtazamo wako… Utabadili maisha yako.