Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Sio Kila Mzee Anafaa Kuombwa Ushauri, Hata Wajinga Huzeeka

Kuna wale wajinga sana au wapumbavu sana pia wanazeekaga

Kuna wale watu walikuwa na tabia za ovyo ujanani nao huzeeka

Kuna wale walikuwa wakorofi, wachonganishi na hata wambea pia nao huzeeka

Kuna wale walikuwa wavivu sana na hawajui kabisa kujituma pia huzeeka

Kuna wale ambao walikuwa wanajali starehe na hata walitelekeza familia zao kisa maisha ya anasa pia huzeeka

Kuna wale wadada hawakujua hata maisha yanatafutwaje kwa njia halali pia huzeeka

Kuna wale walikuwa wapenda njia za mkato na Utapeli huzeeka

Kumbuka hata wale waliokuwa na hofu ya kuwekeza na kufanya maamuzi magumu pia huzeeka

Halafu kuna wale ambao ujanani kwao hawakuwahi kwenda hata nchi jirani au hata mkoa jirani kabisa!

Sasa unapoomba ushauri kwa hawa watu unahisi utapata majibu gani?

Yaani unataka biashara unaenda kumuomba mzee ushauri wa biashara kisa kala chumvi nyingi Ila hakuwahi kufanya biashara yoyote zamani!

Una enda kumuomba mzee Ushauri wa kujiripua nchi ya mbali wakati yeye mwenyewe hata Uganda haja fika!

Una omba ushauri wa ndoa kwa mzee ambae alitelekeza mke wake na watoto ujanani! atakushauri nini?

Unaenda kuomba ushauri kwa mtu ambae aliishi kwa kugombanisha watu na sasa wewe unataka ujue namna ya kuishi na watu vizuri kupitia ushauri wake!

Yaani ushauri wa kuishi na mke au mume vizuri unaomba kwa mzee aliye achika zaidi ya ndoa kadhaa na kila mtoto ana baba au mama ake!

Sawa watakushauri kupitia majuto yao lakini bado hayatoshi kukupa muongozo sahihi

Elewa kuwa hata vijana wadogo wanaweza kukupa ushauri na ukakufaa zaidi ya ule wa wazee

Chagua mtu wa kumuomba ushauri hasa ambae anafanya vema zaidi kwenye jambo unalotaka hata kama bado ana umri mdogo.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Changamoto Hukomaza Akili Na Mwili

Next Post

Mabadiliko Yanaanza Na wewe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.