
Usikubali kuwa wa kawaida wala kufanya mambo wanayofanya wengine na yaliyozoeleka
Mafanikio huja kwa kufanya vitu hata kama ni vidogo vidogo lakini katika njia ya kipekee
Tafuta ladha yako mwenyewe usiige watu wengine
Fanya kwa namna yako ambayo italeta msisimko katika milango ya fahamu ya wateja na mashabiki zako
Wafanye wateja wapate hisia tofauti, ladha ya kipekee na hata waone vitu ambavyo hawaja zoea kuviona kwenye macho yao
Watu waliofanikiwa zaidi sio kwamba ni watu maalumu sana au wenye nyota sana wala wana kibali cha peke yao
Bali walifanya mambo yao katika namna ya tofauti na kipekee bila uoga (ubunifu wa ziada)
Epuka kuwa wakawaida, kama unafanya mambo sahihi na unajua nini unafanya basi USIOGOPE KUONEKANA TOFAUTI.
Anza sasa kujiuliza kwenye hicho hicho kidogo unachokifanya unawezaje kujitofautisha na wengine?
USIKUBALI KUFANANA NA WENGINE UMEUMBWA KUWA WA KIPEKEE.