
Kuna tofauti kubwa kati ya kusubiria lifti chumbani na kutoka kuifuata barabarani
Hata dawa hushika penye kidonda kwa maana kuwa hata maombi na dua hufanya kazi kwenye jitihada
Hakuna muujiza ya usafiri kushuka chumbani hata kama utakesha ukiomba!
Simama na zifuate gari mahala zilipo huku ukiomba Mungu na kuomba lifti kwa wenye magari
Lakini pia huwezi kupata gari za mtwara njia ya kwenda bagamoyo
Lazima ufuate uelekeo sahihi wa njia ya mtwara Ndio utakutana na gari za mtwara hata kwa hatua ndogo ndogo
Hivyo Basi haijalishi ukubwa wa maono uliyonayo,
Kama hautoyafanyia kazi hata kwa hatua ndogo ndogo zenye muelekeo sahihi elewa kuwa hakuna muujiza utakusaidia
Mungu humsaidia anae jisaidia na maombi au dua hufanya kazi palipo na jitihada.
JIWEKE KARIBU NA BAHATI ILI UBAHATISHE.