
Usikubali mazingira yakwamishe ndoto zako wala kukupa vikwazo vya kuwa unavyojiona kwa ndani
Usikubali watu wakwamishe mafanikio yako kwa kukupa sababu za kushindwa
Usikubali mila wala tamaduni zikuwekee vikwazo vya kutimiza malengo yako kisa hadithi za kusadikika
Vuka vikwazo vyote na simama imara wewe mwenyewe
Ondoa sababu zote zenye kuleta pingamizi za kuwa vile unavyotaka
Umeumbwa kwa uwezo mkubwa sana na unapaswa kuutumia kuwa vile unataka
Tengeneza mabaya yako, paa na fika mbali kwa namna unayotaka
Usisubiri kushikwa mkono wala kuongozwa na mtu yoyote yule, vaa uhusika wako
Wewe ni wa thamani sana na una kila kitu ndani yako chenye uwezo wa kukupa unachotaka
Anza sasa usingoje zaidi, muda haukusubiri, paa fika mbali unapotaka.
Great