
Hakuna aliyeletwa Duniani kwa ajili ya kuteseka
Kabla Mungu hajamuumba Binaadamu aliumba Dunia na vilivyomo
Kwa sababu moja tu Binaadamu anapaswa kutawala vitu, sio kutawaliwa
Dunia yote pamoja na vilivyomo, vimeumbwa kwa ajili ya watu (viumbe hai)
Kila kinachofikika kipo kwa ajili ya kutumikia watu
Mazingira yote unayoona na vilivyomo ndani yake, vipo kwa ajili yako wewe pia
Vitawale na tawala Dunia yako
Binaadamu yupo kwa ajili ya kutumikiwa na vitu, sio Kutumikia au kutumika
Ukiona unatumika sana kwa ajili ya maisha ya Dunia elewa kuwa kuna kitu unakosea!
Ukiona unaumizwa sana kwa ajili ya maisha ya Dunia basi tatizo lipo kwako mwenyewe!
Ukiona unakosa raha kwa ajili ya jambo lolote lile kwenye maisha, basi wewe ndio changamoto yenyewe!
Na chanzo kikubwa zaidi cha kufanya maisha yakupeleshe na kukutumikisha, ni kuishi nje ya mstari wako!
Kuishi nje ya mstari wako kabla ya kuchora ramani sahihi ya mstari mwingine!
Kwa sababu ya tamaa na haraka ya maisha ambayo hujaweka utaratibu maalumu wa kufika unapotaka
Kila mmoja ana mstari wake wa maisha na ukomo wa kutumikiwa na Dunia yake
Dunia haitumikii kila mtu kwa namna anayotaka bali kwa kanuni maalumu ya mstari wa kwenye maisha ya mtu husika
Mstari huo husogea taratibu na kumpa nafasi mtu kuishi maisha anayopaswa kuishi kulingana na nyakati sahihi
Nyakati ambazo huambatana na kiwango cha mafanikio yake
Kama utaishi ndani ya mstari wako hakika lazima ufurahie Dunia maana ndio utaratibu unaopaswa kufuatwa!
Maisha yana kanuni zake ukiondoa kanuni zako wewe ulizojiwekea
Na pia ukiona unapitia mateso mengi sana na Dunia inakuwa chungu sana, basi ukweli ni kuwa chanzo ni wewe umevuka mstari kabla ya muda sahihi
Rudi nyuma kwenye mstari wako kwanza kabla mambo hayajawa magumu zaidi
Hakina utaona utamu na ladha ya maisha yako.