
Umewahi kujiuliza kwanini ukinyoosha kidole kimoja kwa mtu, basi vingine hukugeukia wewe?
Hivi unajua kuwa siku zote unapaswa kukagua madhaifu yako kabla ya kukagua madhaifu ya wenzako?
Kuna watu hujiona bora sana, kisha huhisi wengine kama vile hawana maana kama walivyo wao!
Hawa ndio wale ambao kutwa hupambana kutafuta makosa ya wenzao,
Hawa ndio wale ambao huonaga baya kwenye kila afanyacho mwingine
Hupenda kukosoa sana na kuhisi kama wengine hawajui kitu wala hawana akili nzuri
Hujaribu kukagua madhaifu sana badala ya kukagua mazuri ya mtu.
Asili ya maisha inatutaka kabla hatujaona makosa ya wengine basi tuanze kujikagua sisi kwanza
Kabla hujaona madhaifu ya mtu mwingine, anza kukagua madhaifu yako wewe binafsi kwanza
Kabla hujamsema mtu mwingine kwa mabaya basi anza kukagua mabaya yako kwanza.
Usiwe mwepesi sana kuona makosa ya wengine kabla hujaona makosa yako
Tambua kuwa Duniani watu hawafanani na kubwa zaidi watu hawajakamilika.
Hakuna mkamilifu kamwe na kila mmoja kuna namna tu hajatimia kwa asilimia zote kwenye eneo fulani
Hivyo ni vyema kuheshimu na kuhifadhi madhaifu ya wenzetu kwa namna ambayo tungependa madhaifu yetu yahifadhiwe pia.