
Leo nimekumbuka sana maisha ya nyuma na moja kati ya vitu vilivyo nifanya nikumbuke sana ni Rafiki zangu watatu
Kwenye maisha nimewahi kukutana ma watu wengi sana tofauti tofauti
Nimewahi kuwa na urafiki na watu wengi tu tena jinsia na rika aina zote.
Ila nina marafiki zangu watatu ambao waliacha alama kubwa kwenye maisha yangu,
Unajua tumezungukwa na marafiki wengi sana Ila asilimia kubwa huwa nasi kwa ajili ya faida fulani,
Sio kila rafiki ana mapenzi ya dhati kwako
Asilimia kubwa ya marafiki ni wanafki sana hawa ndio wale wakiona umepata huumia mno ndani kwa ndani
Marafiki ambao wanawinda faida tu, siku usipowapa wanachotaka hukubwaga kama uchafu dampo.
- GWAMAKA
Dada huyu sijui nieleze vipi ila alinipenda kwa zaidi ya asilimia 100
Alinipenda wakati sina hata mia, na hakuwahi niomba hata 100 pindi nilipopata maisha
Huyu nimesota nae sana kitaa, enzi hizo hatuna hata pesa ya kula (tumetiana sana moyo kwenye utafutaji)
Nilijua ananipenda Ila sikujua kama ananipenda kwa kiwango kilichopitiliza
Nakumbuka siku ambayo nilifaulu mtihani wa kidato cha 6 (nilienda kumwambia kwake maana tayari alikuwa anaishi na mchumba wake)
Nilivyofika nikiwa nacheka kwa furaha, alihisi tu kuna kitu so nikamwambia nimefaulu mtihani
Aise kwa mara ya kwanza namuona mtu analia machozi ya furaha kwa ajili yangu
Gwamaka hakujibu kitu Ila alibubujikwa na machozi bila kutegemea na ghafla alinikumbatia kwa nguvu sana
Unajua maisha ya urafiki wa uswahili kwanza hatuna mambo ya kukumbatiana, hayo wanafanyaga watoto wa masaki
So ilikuwa mara yetu ya kwanza kukumbatiana halafu pasipo na maandalizi wala kutarajia
Guess how much real friendship feelings ilikuwa pale (yani ile true feelings unahisi kabisa hii imetoka damuni kabisa) mpaka akili ilihama kwa muda!
Gwamaka hata asingenipongeza kwa mdogo yani vitendo tu vilifanya nijue kuwa amefurahia mafanikio yangu kwa moyo wa dhati sana
Nampenda sana Gwamaka she is true friend kwenye shida na raha.
- MARIA
Huyu binti dah sina hata maneno mengi maana alinionesha urafiki wa dhati sana
Nakumbuka siku moja nilichelewa kurudi kutoka shuleni
Unajua kutembea kwa mguu from buguruni to tandika ni bonge la hatua (mbaya sasa mvua ilinyesha kubwa sana siku ile)
Nililazimika kukaa njiani mpaka mvua iishe kwanza maana ilikuwa hatari
Shule nilikuwa natoka sa 1 au sa 2 usiku na mpaka kufika tandika najikuta nafika saa 3 mpaka 4 huko inategemea na namna ntakavyochapulisha miguu.
Maria alikuwa anafunga duka saa 4 kwa ajili ya usalama maana tandika kuna vibaka sana
So siku hio nilijikuta nafika karibia sa 6 usiku (Ajabu nilikuta Maria hajafunga duka mpaka muda ule)
Nilishangaa sana kwanini hajafunga duka (nikawaza labda sababu ya mvua but bado sio sababu kubwa maana vibaka wangeweza vamia kwa wepesi zaidi kutokana na mvua +giza)
Nilifika pale dukani nikakuta Maria kainama, chini ni kama hakuwa Sawa,
Aliponiona alinivamia kwa hasira ni kama alitaka kunipiga kibao but akajizuia
Kwanza nilishangaa sana why yuko vile au nimemkosea Maria!
Wakati naendelea kushangaa na kuwaza haraka nijue kosa langu, ndio akaniambia
“Kwanini umechelewa mpaka muda huu na simu yako haipatikani?” umenifanya nihatarishe kazi sababu yako! Nawezaje kwenda kulala na sijui uko wapi?
Hapo kwanza hata sikuwa nakumbuka kama nna simu (niliizima sababu ya mvua so ilikuwa off kwenye mkoba wangu).
Kabla sijajibu wakati nakagua ili nitoe simu yangu, Maria alinipa sahani ya wali na soda
Eti kwa hasira (Ila najua alinisubiri ili anipe chakula halafu sasa ule wali kumbe aliweka oda kwa ajili yangu mimi na yeye na alitaka tule pamoja)
Dah hahahha kwanza najikuta nacheka maana pia siku ile nilicheka sana
Kumbe hakufunga duka sababu yangu
Maria aliamua kuweka kazi yake hatarini sababu yangu mimi tu
Maria aliamua kupigwa na baridi kwa ajili yangu mimi tu
Maria aliweka maisha yake hatarini usiku wa giza na mvua kubwa sababu yangu mimi tu (imagine vibaka wangevamia pale)
Yote hayo kwa ajili ya mapenzi ya kweli na urafiki wa dhati sana aliokuwa nao kwangu hakika niliumia na kufurahia kwa wakati mmoja.
- EDGAR
Wanasemaga hakuna urafiki wa mwanamke na mwanaume bila kuwa na mahusiano ya kimapenzi nakataa kabisa
Huyu kaka alinipenda sana kama dada na mshkaji wake wa dhati mno
Halafu nikikumbuka sababu ya kujuana nae mpaka leo huwa nacheka tu
Edgar alikuwa dokta, kijana smart na mchapakazi sana
Nakumbuka aliwahi kuniambia “Mwajuma hii Dunia imesha kukataa, so pambana kwa vyovyote vile utobe”
Unajua kwanini aliniambiaga vile.. Ni sababu ya changamoto nilizowahi kupitia kwenye maisha yangu
Edgar alikiri kabisa yeye hajawahi pitia maisha kama yangu na kama angepitiaga basi asingeishi!
So alikuwa bonge la mshkaji sana aise na siri zangu nyingi alikuwa nazo yeye (hata Maria na Gwamaka hawajui vitu vyangu ambavyo Edgar anajua)
Edgar alitaka kunipa nyumba yao ya urithi nikae bure wakati najitafuta (hii nyumba ilikuwa chamazi mpya Ila haijaisha baadhi ya vitu) baba yake aliijenga mwaka mmoja kabla ya kufa kwake so ilikuwa mpya kabisa
Ila sikuweza kukaa kule sababu ya umbali na ilipo kuwa kazi yangu (kazi nilikuwa nafanyia banana ukonga pale AVIATION) wakati nimekosa mkopo wa chuo.
Huo niliona ni zaidi ya upendo wa Edgar kwangu, mtu ambae tulijua mjini na tukaamininiana sanaa.
So urafiki wa kweli siku zote kwanza hauna mipaka ya mapenzi
Urafiki wa kweli huja wenyewe automatic
Urafiki wa dhati hautaki sababu za msingi za kupendana
Urafiki wa kweli siku zote upo natural tu huja bila kutumia nguvu
Na urafiki wa kweli haunaga kipimo wala mashaka ndani yake
Ukiona una rafiki Ila kuna namna unahisi mapungufu ya urafiki wenu tambua kuwa haupo kwenye urafiki sahihi.