
Kwenye maisha kuna nyakati unaweza kupoteza vitu vingi sana
Vinaweza kuwa vya thamani kubwa au hata thamani ndogo
Pia vinaweza kuwa vitu au watu..
Kuna muda unaweza poteza kwa bahati mbaya au kwa kukusudia
Na kuna vile hupotea bila kutarajia au kwa sababu za watu wengine
Kitu cha msingi zingatia kilichobaki karibu yako au kwenye himaya yako
Usiumizwe kabisa na vile vilivyoondoka hata kama ulikuwa na mapenzi navyo sana
Kama kitu kimepangwa kuwa chako kitakuwa tu na kama hakijapangwa haijalishi utakilinda kiasi gani kitaondoka tu!
Usipoteze muda na nguvu zako kuchota maji yaliyomwagika!
Kuna uwezekano mkubwa upata madhara kupitia uchafu wake na uhakika ni kuwa hutopata maji kiasi au ubora kama wa mwanzo
Zingatia maisha uliyo nayo kwa kuangalia wanao kushikilia au hata unavyo miliki kwa sasa
Kitu chochote kinacho ondoka hakika kimepangwa kuondoka na kuna uwezekano ukapata kilicho bora zaidi
Acha viende, acha waende! Kama utabaki na afya au pumzi yako basi inatosha kukupa zaidi ya vile
Jiulize mwanzo kabla yao au kabla ya hiko kitu uliishije? Au ulikipataje mpaka ushindwe kupata kingine?
Hivyo epuka maumivu ya kujitakia kumbuka kila kinacho kuepuka kina kheri na wewe.