Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Usikubali Furaha Yako Imilikiwe Na Mtu Mwingine

Jitahidi sana furaha na amani yako vikutegemee wewe mwenyewe

Usikubali kabisa furaha yako iwe kwa mtu mwingine wala kitu kingine

Yani unapaswa kuwa chanzo cha furaha yako bila utegemezi mwingine wowote

Bila kujali mazingira uliyopo kwa sasa au kwa baadae

Bila kujali watu wanao kuzunguka sasa au hata baadae

Na bila kujali vitu unavyo miliki sasa au hata baadae

Kwa maana kwamba hata kama kitu, watu au mazingira vikibadilika basi wewe unapaswa kubaki vile vile

Ikitokea umesalitiwa na kuachwa na mtu yoyote unapaswa kubaki vile vile

Endapo utabadili mazingira yako kwa namna yoyote ile unapaswa kuwa na furaha ile ile

Na ikiwa utapoteza kitu chochote hata kama ni kitu cha thamani sana unapaswa pia ubaki na furaha ile ile

Yaani hupaswi kabisa kuishi kwa ajili ya kitu, mazingira au mtu

Elewa kuwa watu wana badilika muda wowote na vitu vinaweza kupotea wakati wowote pia mazingira hubadilika wakati wowote!

Usiwe mtu ambae utapoteza muelekeo wako kisa watu wengine, mazingira au vitu vingine

Furaha yako inapaswa kutoka ndani yako wewe mwenyewe

Ndani ya moyo na roho yako bila kusahau mwili wako

Jipende kiasi kwamba huhitaji mtu mwingine kukusaidia upendo ili kujiona umekamilika

Jipende kwa kiwango kuwa hata kama utapoteza kila kitu na kuanza upya kabisa bado hutoweza kujipoteza wewe mwenyewe

Jipe furaha kwa kadiri unavyoweza hata kama itagharimu kila ulichonacho

Ila kamwe usipoteze chochote kwa ajili ya mtu mwingine kukutunzia furaha yako.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kuna Wakati Amani Ni Bora Kuliko Ushindi

Next Post

Kwenye Maisha Hakuna Anae Wahi Wala Anae Chelewa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Tafuta Upekee Wako

Usikubali kuwa wa kawaida wala kufanya mambo wanayofanya wengine na yaliyozoeleka Mafanikio huja kwa kufanya…

Huruhusiwi ku copy makala hii.