
Nilipokuwa na umri kati ya miaka 9 mpaka 15 mama alishindwa kunilea kutokana na ugumu wa maisha
Mbaya zaidi baba yangu nilimuona mara mbili tu katika kipindi cha uhai wake na hata sikumbuki sura yake tena.
Nililelewa na ndugu zangu upande wa baba yangu huko kigoma kasingirima
Babu alinichukua baada ya kuona mama hawezi kumudu gharama za kunilea kwa wakati ule
Hio ilikuwa baada ya mama kushindwa kuninunulia dawa za shillingi elfu 1000 tu kwa wakati ule na hali yangu ilikuwa mbaya kwa homa kali
Mara baada ya Babu yangu kufariki, maisha yalikuwa machungu sana
Mateso na manyanyaso mengi mno nilipitia kutoka kwa ndugu zangu wale
Kuna wakati shangazi yangu ALINIMWAGIA KOPO LA MATE YAKE (alikuwa mjamzito hivyo kutema mate kwenye kopo)
Fikiria mate ya usiku mzima aliyohifadhi kwenye kopo alinimwagia mimi asubuhi
Kosa likiwa kutopika chai kwa wakati kutokana na wingi wa kazi za pale nyumbani!
Mengi yalitokea magumu na mazito sana kiasi kila nikikumbuka huwa napata maumivu makali sana
Kupigwa ilikuwa kawaida mno na hata kutukanwa matusi mazito mno nilizoea
Kuna siku baba yangu mdogo aliwahi kunipiga fimbo nyingi sana huku akinikokota kama mwizi kuanzia chumbani mpaka nje ya uwanja
Nilikuwa kwenye siku zangu za kike, hakujali kabisa namna ambayo damu zilimwagika kila alivyo niburuza
Licha ya wingi wa watu waliozunguka nje kushuhudia navyopigwa na uwepo wa jinsia za kiume hakujali wala kuona huruma!
Kosa lilikuwa kulala mpaka saa 2 asubuhi kwakua nilisema naumwa sana tumbo la hedhi
Mbali na kufanya kazi nyingi sana za nyumbani, hakuna aliyejali wala kuona mazuri yangu
Licha ya kujituma na kujitoa kwa nguvu zangu zote hakuna aliye hesabu kabisa
Sikuwa binti pekee pale nyumbani, kulikuwa na mtoto wa babu umri sawa na wangu ambae nilimwita shangazi
Mama yake (bibi) yangu hakutaka mwanae afanye chochote kile na hata alipokosea hakuadhibiwa kabisa.
Lakini kwa nje walitangaza kuwa wananilea na kunisaidia maisha na masomo yangu!
Naweza kusema moja kati ya kumbukumbu zangu mbaya za utoto zilianzia pale kwenye ile nyumba
Japokuwa walikuwa ndugu zangu wa damu Ila walinitesa kama mtu baki
Na mpaka sasa kigoma ni moja kati ya mikoa ambayo hunipa kumbukumbu mbaya sana,
Kila napo fikiria kwenda hupata wakati mgumu mno hata kukaribia ile nyumba
Japokuwa ndio nyumbani na asili yangu ipo kule
Na hata ninapo amua kwenda kutembea siku zote huwa nafikia nyumba za kulala wageni!
Unaweza kumfanyia mtu mabaya kwa kisingizio kuwa una msaidia
Ukampa msaada kweli lakini msaada uliojaa maumivu
Yule mtu atavumilia sana kwakuwa anahitaji kujikwamua sio kwakua anafurahia unachofanya
Na siku akipata nafasi ya kutoka hapo kamwe hawezi kumbuka msaada wako kabisa
Unaweza kusema ulimlea mtoto Ila baadae amepata maisha yake na hakumbuki fadhila
Kumbe ulimpa fadhila mbaya zilizojaa maumivu makali mno
Kama umeshindwa kumlea au kumsaidia mtu bila manyanyaso ni bora muache aende kuliko kumjengea kumbukumbu mbaya kichwani kupitia msaada wako
Watu wengi sana hupitia mateso mengi kisa misaada wanayopewa
Baada ya muda huja kulipiza mabaya hata kwa vitendo kisha watu hutangaza kuwa alisaidiwa na kalipa ubaya
Kumbe wema aliopewa ulificha ubaya kwa ndani toka mwanzo kutoka kwa walomsaidia.