
Usiogope kujaribu jambo hata kama unahisi huliwezi au ni gumu sana
Kataa kabisa neno haiwezekani kwenye akili yako hata kama lina ukweli ndani yake
Siku zote jitahidi kujaribu vitu vingi na kuwa mdadisi mara kwa mara
Kila unapo lazimisha kujua kitu Ndio njia ya kujifunza zaidi na kuwa bora
Wakati mwingine kuna uwezekano hiko kidogo unachokiweza ndio jibu na njia sahihi zaidi au hata hakuna mwingine anaeweza kama wewe kwa wakati huo!
Ubunifu upo kwenye kujaribu mambo tofauti tofauti na mafanikio yapo kwenye ubunifu…
Hivyo kila kinachokuja upande wako kama hakina madhara makubwa na kinahitaji kufanywa na wewe usikubali kusema siwezi,
Badala yake jitutumue Jaribu kidogo, jifunze na ukiweza uliza wengine kinafanywaje? Ila kamwe usiseme HAPANA.