
Watu wengi sana kwa sasa imekuwa kawaida sana kuomba Msaada kwa wengine
Kitu ambacho sio jambo baya sana na wala sio jambo jema kabisaaa
Ubaya unakuja pale ambapo mtu huyu huyu anataka msaada wa muda mfupi
Lakini hataki hata kusikia kufundishwa kuingiza kama zile anazoingiza muombwaji
Yaani anataka umpe pesa au kitu cha thamani lakini hata mara moja hajawahi kuumuliza huyu huyo mtu nifanye nini niwe kama wewe
Hataki hata kusikia mchongo ulivyo wala mchakato unavyoenda Ila anataka apewe chochote kitu tu
Halafu akinyimwa anajenga chuki na ubaya kwa mtu tena bila aibu kabisa
Hujui magumu mangapi wenzako wanapitia kwenye utafutaji
Hujui kuna muda wanakesha na hata wanapata maneno makali kwa mabosi zao au wateja
Hujui hasara ngapi wanapata na hata maumivu kiasi gani wanayo
Huelewi kabisa hata wamepoteza pesa kiasi gani kwenye kupata hiko walicho nacho
Unachojua ni kuomba tu kirahisi kama vile ni chako wewe au umewekeza kwao
Halafu ukinyimwa unaanza kutangaza ubaya kwa mtu!
Mbaya zaidi ukiambiwa njoo na wewe ufanye hiki upate pesa unasema bila aibu kabisa eti hayo mambo yenu mimi siwezi!
Au sina muda kuna inshu nafanya… Ajabu izo inshu hazikupi chochote
Yani wewe una lala ndani wenzako wanakesha usiku na jua la mchana halafu kirahisi tu unaomba kuungiwa mazaga!
Hebu badilika siku moja na wewe useme chukua hii.. badala ya Naomba hii
Yani na wewe uwe unatoa kwanza ujue uchungu wa kutoa kitu.