
Pinga hali ya kuogopa na ikatae kwa nguvu zotee
Kataa hali ya kusita kufanya jambo kwa uwezo wako wote
Usiruhusu akili yako ikuoneshe vikwazo na changamoto badala ya maarifa yakinifu
Pinga kabisa kubaki nyuma, kujishtukia na kujiona dhaifu
Duniani tunaishi mara moja kwahio tumia muda wako vyema
Hakuna ugonjwa wa hofu wala aibu bali wewe mwenyewe Ndio umechagua kubaki salama ukiogopa kuchekwa endapo utashindwa kwenye kitu fulani
Kushindwa ni kawaida wala wewe sio wa kwanza, ni bora ujaribu ushindwe uchekwe kuliko kufurahisha watu kisha kuchekwa utakapokuwa omba omba
Watu wanaokucheka leo, watakucheka hata kesho kwakuwa utakuwa umechagua kuona upande wa vicheko vyao
Vaa miwani nyeusi, jifanye kipofu na weka ujasiri kisha anza kufanya hicho kinacho kugopesha.