
Wakati unahangaika kutafuta maisha yako unayotaka
Ndio wakati huo huo pia unapaswa kuishi maisha unayotaka
Kila kilicho original kina kopi yake na kila kilicho kamilika kina summary yake
Hivyo unaweza kugeuza maisha unayotaka kuishi baadae, ukayaishi sasa kwa namna tofauti!
Usingoje mpaka umiliki vitu fulani ndio ufurahie maisha yako
Furaha hupaswa kuwa sehemu na mazoea ya maisha unayoishi kila siku haijalishi kiwango cha mafanikio uliyonayo
Ishi wakati unatafuta maisha, usisubiri kitu chochote
Badili mtazamo wako kwa namna tofauti na utaona muujiza mkubwa sana wa raha ya maisha
Kuna watu wana mafanikio makubwa Ila hawana amani wala raha ya mafanikio yao
Watu hao hao kabla ya kufanikiwa walisema, “siku nikipata mafanikio fulani nitakuwa na furaha sana”
Ajabu ni kuwa mafanikio wamepata Ila furaha na amani hawana kabisa.
Kuishi wakati unatafuta maisha yako ni neno lenye maana pana sana
Lakini kwa ufupi ni kuwa hakikisha kila giza linapoingia uwe umekamilisha maana ya siku nzima uliyoishi siku hio
Jitahidi kabla hujalala ujione kabisa siku yako imeenda vile umetaka na huna deni na maisha yako kabisa
Lakini pia jitahidi umiliki furaha yako bila kujali changamoto unazopitia
Na usisahu kujipa raha kwenye hiko hiko kidogo unachopata
Wala usiendekeze shida na mahitaji ya maisha maana huwa haviishi kamwe!
Ishi maisha makamilifu unayotaka kuyaishi bila kujali kiwango cha mafanikio yako
Ukipata muda wa kufurahia basi furahia kama vile hutofurahi tena
Na ukipata nafasi ya kutumia basi tumia, jiachie kama vile tayari umemaliza shida zako zote, Ila hakikisha huharibu bajeti yako!
Sio lazima uwe serious sana na maisha, hujaumbwa kuteseka
Hata Mungu hufurahi na kutoa zaidi kwa wale ambao huonesha hali ya kuridhika na kufurahia kidogo wanachopewa!
Badili matazamo wako hakika Dunia ni sehemu tamu sana.