Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Usisahu Kujenga Maisha Yako Binafsi, Wakati Unajenga Maisha Ya Familia Yako

Kuna uwezekano mkubwa sana nyumba unayo jenga sasa kwa ajili ya watoto wako, Wataiuza siku chache baada ya kifo chako

Namna unavyojinyima kwa ajili ya maisha ya kesho ya familia yako, kuna uwezekano mkubwa kila ulichowekeza kikauzwa kwa bei ya hasara kubwa siku chache sana baada ya kufa kwako!

Eneo unalo nunua sasa kwa lengo la maisha ya watoto wako kesho, kuna uwezekano mkubwa hata wasipapende na wakataka kuishi mahala pengine kabisa!

Njaa unayo vumilia sasa pengine hata unapata vidonda vya tumbo ili ujengee wanao maisha ya kesho, kuna uwezekano mkubwa kila kitu kikamilikiwa na watu wengine kabisa hata usiowategemea na wanao wasijuie hata thamani ya kila ulichoacha!

Usisahau kuwa Familia unayo pambania kuipa furaha sasa, kuna uwezekano mkubwa sana wasikumbuke fadhila zako baadae

Usishangae muda wa wewe kutunzwa, watoto wako wa damu watakuacha kama ulivyo bila huruma kabisa

Watathamini wenza wao waliokutana nao ukubwani na wewe uliyewazaa utabaki kijijini bila msaada!

Usishangae watoto 10 unaowatunza sasa, ukakosa hata mmoja wa kukusaidia au kukunulia hata panado tu kwenye maisha ya baadae!

Hivyo usijisahau sana wakati unaandaa kesho ya wanao au familia yako

Usijinyime sana kisa maisha ya wanao ya baadae, ukajiacha nyuma

Weka 10 kwao tunza moja kwako!

Ukinunua nguo 10 za mwenza wako au wanao basi na wewe nunua moja kwa ajili yako

Ukitenga milioni 2 za akiba ya wanao, na wewe tenga elfu 50 zako binafsi

Ukijenga au kununua eneo kwa ajili ya wanao hakikisha kuwa sababu kubwa ya kujenga ni wewe kwanza kabla yao

Ukiacha nyumbani laki moja ya matumizi, na wewe tumia elfu 10 binafsi kujipongeza.

Kiufupi jenga maisha yako, wakati una jenga maisha yao!

Fikiria kesho yako, wakati una fikiria kesho yao!

Ifike mahala usibaki na majuto yoyote hata kama mambo yatabadilika basi usiwe umeishi kwa ajili yao pekee

Maisha yako ni yako na yao ni yao japokua jukumu la kuwatunza lipo kwako!

Siku ukifa, utasahaulika kwa kila jambo na hata magumu uliyopitia utazikwa nayo mwenyewe!

Maumivu na uchungu wa kutafuta kwa ajili yao utakufa navyo wewe!

Kwao itabaki historia ya mara moja moja sana tu kuwa mzazi wangu alinisaidiaga sana au hata usikumbukwe kabisa.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kuna Kumbukumbu Za Maisha Hazina Ufutio, Chunga Tamaa Zako

Next Post

Kuteseka Sana Leo, Sio Tiketi Ya Kufurahia Maisha Ya Kesho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.