Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Uzito Wa Hoja Hupimwa Kwa Hoja Nzito Zaidi Kwa Maana Hakuna Mzani Wa Hoja

Kuna watu wakishapata Elimu kiwango fulani basi huamini kuwa wamemaliza kila kitu,

Hawa ndio wale ambao hujawa viburi na majivuno hata wawapo kwenye nafasi kubwa zaidi ya wengine

Watu kama hawa huwa wabishi sana hata pale wanapokosea hukataa kabisa kutolewa kasoro

Wanasahau kuwa unapaswa kubisha hoja kwa hoja nzito zaidi.

“Ngoja nikupe mfano mmoja mdogo hapa…

Binafsi nilihisi najua sana kupika ugali baada ya kufundishwa na Bibi yangu kigoma,

Bibi alikuwa bingwa wa mapishi pale nyumbani hivyo wanafamilia wote tulimkubali sana.

Mara nyingi nilikuwa mpishi wa ugali na hakuna aliyewahi kula ugali wangu kisha kuutoa kasoro mpaka siku niliyoenda kijiji kimoja hivi huko wilaya ya kibondo.

Nilienda kwa rafiki yangu Mwalimu, pale nilikuta anaishi na Mwalimu mwingine kwenye kota yao,

So walikuwa walimu jumla wawili (rafiki yangu hakuwa na familia ila yule Mwalimu mwingine alikuwa na mke, mtoto mmoja na mdogo wake wa kiume)

Huyu mdogo wake alikuwa na umri kati ya miaka kama 14 au 15 hivi yaani alikuwa mvulana mdogo tu tena amekulia maisha ya kijijini.

Siku moja mke wa yule Mwalimu aliondoka hivyo tukabaki sisi wawili, Mwalimu na mdogo wake tu (jumla 4)

Tukaamua tupike chakula tule pamoja kama namna yakuongeza kampani.

Hivyo mimi nilijitolea kupika mchana ugali na dagaa,

Niliamini nimepika vizuri sana kwa sababu najiamini najua kupika, (ajabu yule mdogo wa Mwalimu alitoa kasoro kwenye ugali wangu)

Akasema eti wadada wa mjini hatujui kupika na hata akikua ataoa msichana wa kijijini kwao.

Ukweli nilishangaa sana kwa mtoto kama yule kuongea vile huku anajiamini kama mtu mzima (wakati mimi najiona fundi jikoni).

Nilipomuuliza kwani ugali una kasoro gani?

“ndio akasema ngoja usiku nitapika mwenyewe uone kasoro kati ya ugali wako na wangu”.

Kweli usiku tena tuliamua kupika pamoja kwa maana mke wa yule Mwalimu hakurudi,

Kama alivyoahidi yule mtoto kweli alipika, ugali na matembele.

Aise unajua kwanza sikuamini kama yule mtoto anaweza kupika ugali mzuri zaidi yangu, kwahio nilikuwa nafualitia hatua kwa hatua toka anaanza maandalizi,

Na kweli niligundua jambo ambalo sikuwa nafanya kwenye mapishi yangu ya ugali

Unajua ile tumezoea ugali hauna maajabu sana kwenye upishi wake kwa maana hatua ni zile zile tunazofuata.

Yaani kubandika maji, kisha kukorogea uji na baadae kusonga ugali basi.

Ila huyu alifanya tofauti kidogo na ugali ulikuwa mzuri sana (ugali unaweza kula hata bila mboga na bado ukafurahia)

Yaani ugali ulikuwa mzuri kiasi kwamba hata ukila huwezi kutamani kushiba kabisa, kuanzia tonge la kwanza hadi mwisho joto lake halipoi wala utamu haupungui.

Nilikubali kushindwa na nikajiona mgeni sana mbele ya mtoto mdogo kama yule tena mtoto wa kiume.

Niliamua kuanza kupika ugali kama wa yule mtoto na kweli nilianza kuona mabadiliko kwa watu wanao kula ugali wangu

Mara zote yoyote anaekula ugali wangu haachi kusema jambo kuhusu utamu wa ugali.

Ugali ambao napika kwa sasa ni tofauti na ule wa zamani

Kila anae kula ugali wangu basi hutamani nipike tena na tena.

Hivyo ndivyo nilipata Elimu mpya ya ugali kutoka kwa mvulana mdogo wa kijijini ninayo itumia mpaka sasa.

Kwenye maisha usidharau mtu kwa umri, mazingira wala kipato chake,

Yule mtoto ameniongezea somo kubwa sana ambalo nalitumia kwenye mambo yangu mengine,

Kukubali kushindwa ninapo kosolewa hata kama ni kitu nilichozoea kufanya miaka ya nyuma

Haijalishi najua kitu kiasi gani, anapotokea mtu kunirekebisha basi nami hukubali kushuka kwanza kisha kuangalia utofati wake na wangu,

Bila kujali umri wa mtu huyo, mazingira yake wala uchumi wake!

Kitu pekee ninacho zingatia ni wapi nakosea na wapi yeye amenizidi halafu nikiona makosa yangu hujirekebisha na kushukuru.

Hii inanipa uwezo wa kuboresha mambo mengi sana ninayofanya mara kwa mara.

Hivyo usiwe mbishi sana unapopewa maelekezo na wengine,

Wala usijafanye mjuaji kudharau wengine kisa umri au mazingira yao

Na wala usijikute unajua sana kuliko wengine hata kama umewazidi Elimu na cheo,

Tambua kuwa unaweza kujifunza chochote kwa mtu yoyote wakati wowote ule.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Unapo Nyoosha Kidole Kimoja Kwa Mwingine, Kagua Uelekeo Wa Vidole Vilivyobaki

Next Post

Hakuna Tuzo Za Kelele, Unapotaka Kuondoka Kwenye Maisha Yao Basi Ondoka Kimya Kimya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.