
Mungu ana wahitaji wengi sana wanaotaka msaada wake
Kila muhitaji ana sababu za msingi kuliko mwingine!
Kuna wahitaji wana maradhi ya muda mrefu
Kuna wengine walemavu wa kudumu
Kuna wale toka wazaliwe hawajawahi kupona kabisa
Kuna ambao walipata matatizo ya kusababishiwa na hawana kosa lolote
Wapo ambao ukiwasikiliza utaishia kulia kuliko wao wanavyolia!
Kuna watu toka wamezaliwa hawajawahi kuonja ladha ya furaha wala raha
Halafu kuna wale njaa kwao ni kama mseto tu, hata wakipata shibe tumbo linashtuka!
Na wengine kibao ambao wana matatizo na changamoto za kila aina ngumu sana na nzito mno za kiuumbwaji.
Sasa hawa wote kila sekunde huomba msaada kwa Mungu kila mmoja kwa namna yake
Unahisi Mungu anapaswa kumsaidia nani kati yao na wewe?
Chunguza shida zako halafu linganisha hata na shida za wachache wahitaji kuliko wewe unao wajua…
Ndio utagundua kuwa hupaswi kuomba wala kulilia msaada wowote kwa Mungu zaidi ya kupambana na changamoto zako
Hata kama Mungu atakupa unachotaka muda huu, baada ya siku chache utaomba kingine!
Binaadamu hajawahi kuridhika ukizingatia changamoto haziwezi kuisha kamwe!
Kila utakachomiliki au kupewa kina changamoto zake..
Ukiwa mtu unaetaka msaada wa Mungu kwa kila changamoto, utaishia kukosa raha na kukufuru kila siku!
Badala ya kuomba msaada wa kitu fulani kwa Mungu, muombe akupe ujasiri kwa kila changamoto na matatizo unayo kutana nayo
Akupe nguvu na ujasiri wa kupambana na kila mtihani utakaokuja mbele yako
Akupe roho ngumu na ubishi wa kutokata tamaa
Akupe urahisi wa kuona njia na utatuzi wenye busara kwa kila jambo
Hilo peke ake linatosha kukufanya uishi maisha ya amani, furaha na kuiona Dunia katika jicho Chanya.