
Umeshawahi kujiuliza kuwa, toka umeanza kufikiria kufanya kitu fulani mpaka sasa kama ungekuwa umefanya kwa vitendo ungekuwa umepiga hatua gani?
Toka ule mwaka ambao ulisema utaanza kufanya kitu fulani, kwa mfano sasa ungefanya kweli! Je ungekuwa umepiga hatua zipi mpaka sasa?
Unaona namna siku zinavyoenda kasi sana? Unaona namna miaka inavyoenda kasi mno!
Anza kuhesabu sasa imepita miaka mingapi toka ulipoanza kufikiria kufanya kitu halafu hukufanya.
Ondoa visingizio vyote na chukulia ungeanza hivyo hivyo kigumu gumu tu, je ungekuwa na hatua gani hadi leo?
Simaanishi ungekuwa na mafanikio makubwa sana, Ila wewe mwenyewe hesabu faida ambazo ungekuwa umepata kama ungeanza wakati ule bila kuacha.
Inawezekana ni biashara fulani ulitaka kufungua ila ukaghairisha
Au ni wazo fulani ulitaka kutekeleza Ila ukapotezea
Lakini pia labda ni akiba ndogo ndogo ulitaka kuanza kuweka Ila ukagairi
Na pengine hata ni mahusiano ulitaka kuanzisha Ila ukaona muda bado
Au tuseme ulitaka kuanza kujenga mwili kwa mazoezi madogo madogo Ila ukaacha tu
Na hata labda ulitaka kuwekeza kwenye kitu fulani kizuri chenye faida Ila tu ukaona uache bila sababu za msingi
Na labda ni Elimu au ujuzi fulani ulitaka kujifunza ila ukagairi tu pasi na sababu za maana.
Sasa hayo yamepita na huna namna yoyote kurudisha siku nyuma,
Ila unaweza kuanza upya sasa hivi kwa namna hio hio uliyonayo kwa sasa
Anza usiogope kabisa, hujachelewa na unaweza kubadili kila kitu miezi michache ijayo
Amua tu kuwa kuanzia muda huu utafanya kitu chako na kamwe hutoacha mpaka uone faida unayotaka.
Leo unaweza kudharau sana Ila kwa namna siku zinavyokimbia utashangaa miaka 2 inaisha ukiwa hujafanya tena!
Usiogope wala kujiona umechelewa anza upya sasa,
Lakini pia usidharau tena kama nyuma, kwani inawezekana usipate wakati mwingine kama huu tena.