
Zingatia alama za nyakati kabla hujalaumu ugumu wa mambo na changamoto za maisha
Usilazimishe kufanya kitu kinachokukataa kwa wazi
Sio kila nyakati zinafaa kufanya au kutenda kitu fulani hata kama kina umuhimu mkubwa
Kuna muda unaweza kupitia changamoto na maumivu mengi kwasababu tu haupo kwenye nyakati zako
Kila jambo lina alama zake na muda wake wa kutendeka
Ukiona vikwazo ni vingi zaidi kuliko kawaida basi usilazimishe kufanya kitu hata kama una kihitaji sana maana utaishia kupata majuto na maumivu makali bila mafanikio au hata ukafanikiwa baada ya jasho la meno kutoka wakati lilikuwa jambo dogo tu
Acha upepo mbaya upite kwanza kisha fanya wakati mwingine…
Kuna nyakati mambo huenda yenyewe bila kutumia nguvu kubwa sana
Sio kwamba mafanikio ni marahisi sana au hata magumu sana bali ugumu na urahisi wake upo katika alama sahihi za nyakati unazo pitia,
Hivyo anza kusoma alama zako za nyakati na zihusishe katika mambo unayofanya kila siku
Alama za nyakati Ndio zimebeba siri kubwa sana ya mafanikio bila mateso!
Je unazijua alama zako za nyakati? Kama hapana anza sasa kuzichunguza.