
Yaani mchakato mzima wa upatikanaji wa mimba watu huwa hawaulizi
Mateso yote ya mimba na mahangaiko yake hakuna atakae taka kujua
Shida za mimba, na hata dawa ulizotumia kupata mimba wala watu hawajisumbui kutaka kujua!
Mahudhurio ya kuona madaktari na hata maumivu yote ya kukosa mimba hayupo anae ya hisi zaidi yako
Kuna wale wenye shida na changamoto za uzazi ambao hupitia kebehi na hata matusi mazito kwa walimwengu bado maumivu hubaki kwa mbeba mimba baadae
Hakuna atakae kuwa na wewe na kuhisi mchakato mzima uliofanya kupata mimba
Hakuna atake sema ngoja nikusaidie mateso yako ya mimba
Wala hayupo atae hisi maumivu yote ya kutapika na kushindwa kula kila wakati
Wote husubiri kuona matokeo! Matokeo ya tumbo lilikotuna mbele yako…
Hakika nakuambia hata hayo unayo pitia sasa hivi kuna watu wanaona kama unacheza tu
Wengine wanaona kama umechanganyikiwa tu
Na hata kuna wale hawataki hata kujisumbua kujua unachofanya..
Wote wanangoja siku ufanikiwe wapige makofi ya pongezi!
Kaza moyo safari ya mafanikio haijawahi kuwa rahisi sana wala haipaswi kuwa ngumu sana
Wote ambao huwaoni sasa bado hutowaona ukishindwa!..
Lakini wakisia tu umefanikiwa utashangaa hata uliodhani wamekufa kumbe wapo hai.
Kichwa cha makala kinachekesha ila ni kweli kabisa 🤓
Hahaha hahaha
Bookmarked ✍️
🙏