Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Ukitaka Kufanikiwa Bila Kuchoka Fanya Kitu Unacho Kipenda Sana

Fanya kitu unacho kipenda zaidi ili kikupe hamasa ya kuendelea

Ni ngumu sana kuendelea kufanya kitu ikiwa huna mapenzi nacho ya dhati

Katika harakati za kutafuta mafanikio jitahidi kuchagua jambo unalo penda zaidi

Hii itakupa wepesi hata pale mambo yanapokuwa magumu sana

Kuna zile nyakati hali inakubana mpaka unatamani kuacha kabisa

Ila ukiwa na mapenzi makubwa na kitu hakika hukufanya upate nguvu upya mara kwa mara

Yaani angalia jambo gani ukilifanya hata kama hutopata faida haraka bado huwezi kulichoka

Chagua kitu ambacho kila ukifikiria kukiacha unaona ni kama umepoteza maana nzima ya kuishi kwako

Fanya jambo ambalo hata kama utakosa shabiki au mteja bado unaweza kujishabikia mwenyewe

Iwe biashara au hata kipaji, ikiwa utakipenda kwa dhati hakika huhitaji mtu mwingine aje kukuambia neno lolote ili upate nguvu

Kitu kikitoka moyoni utajikuta wewe mwenyewe una jishauri na kurekebisha makosa yako hata kama huna mshauri

Hutongoja hamasa ya nje ikupe nguvu ya kuendelea pale unapokwama na kukosa nguvu

Hutotaka kusikia mtu anakuambia acha hakina faida unapoteza muda

Hutoshawishika na tamaa zingine zozote zinazoweza kukutoa nje ya lengo lako

Lakini pia utajikuta unaacha kila kitu kwa ajili ya jambo lako

Utatengeneza mazingira ya kufanikisha hata kama kuna ugumu

Utajikuta bila kutarajia unapata njia na mawazo chanya ya kufanikisha unachotaka

Msukumo wa mapenzi kutoka ndani hutoa nguvu ya ajabu sana kwenye harakati zako

Hutokuwa na kisingizio cha kuamka asubuhi na hata kukesha kwa ajili ya jambo hilo

Na bado utakilinda kwa moyo wote hata kama itatakiwa kutoa kila ulicho nacho kwa ajili ya jambo lako

Na hata kama utafika ukingoni kabisa mwa mawazo na akili ya kufikiria bado uta kuwa king’ang’anizi kwenye hilo jambo

Na mwisho wa siku mafanikio yatakuja kwakuwa tu hukuishia njiani.

Fanya unachopenda sana hakika nacho kitakupenda.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Usihangaike Na Ulivyopoteza Zingatia Vilivyobaki

Next Post

Mafanikio Ni Kama Mimba, Kila Mtu Hukupongeza Akiona Tumbo Kubwa

Comments 23
Leave a Reply to Onesmo Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.